PETER BANDA AISHIKA PABAYA SIMBA, ATAKA MAMILIONI KUVUNJA MKATABA

Menejimenti ya Royal Soccer Scout Management inayomsimamia Winga wa Klabu ya Simba,Peter Banda imeuambia Uongozi wa Simba kuwa hautaki mteja wao apelekwe kwa mkopo Klabu yoyote ile na badala yake ni kuchagua kumvunjia Mkataba wake na kumlipa pesa zake au kumhakikishia nafasi ya kucheza mda mwingi kuelekea Msimu ujao.

Banda ambaye kwa sasa yupo nchini kwao Malawi anaamini uwezo wa kucheza kwenye Kikosi cha Simba upo ndio maana anashinikiza kuvunjiwa Mkataba ili akacheze sehemu Nyingine au kuhakikishiwa nafasi ya kucheza hali ambayo imewagawa viongozi wa Simba na kushindwa kuafikia maamuzi juu yake.
.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA