Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2026

Simba nje Kagame Cup ikishinda 2-1

Picha
Timu ya Simba SC imefanikiwa kuambulia ushindi kwenye kombe la Kagame Cup baada ya kuifunga Singida Black Stars mabao 2-1 uwanja wa Amahoro jijini Kigali Rwanda. Mabao ya Simba yamefungwa na Ibrahim Doumbia dakika ya 27 na Elie Mpanzu dakika ya 66 wakati goli la Singida lilifungwa na Mathew Tegisia Momanyi dakika ya 55 na timu zote zimeaga mashindano hayo kufuatia pointi zao hazikuivuka Jamus ambayo imeingia nusu fainali kwa kufikisha pointi 7

Kocha wa Bafana Bafana ajiuzuru

Picha
Kocha Hugo Broos amejiuzulu nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) baada ya kuhudumu kwa miaka mitano!. Hugo amejiuzulu baada ya kumalizika kwa michuano ya FIFA World Cup 2026 na Afrika Kusini wapo wanatafuta mbadala wake mapema sana.

Fred Ngoma ni mwananchi

Picha
Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji namba 6, Fred Duval Ngoma, raia wa Jamhuri ya Congo Brazzaville, akitokea klabu ya Olympique de Safi inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco Botola Pro. Ngoma, mwenye umri wa miaka 28, anatajwa kuwa miongoni mwa viungo wenye uwezo mkubwa wa kucheza mbele ya safu ya ulinzi kutokana na uwezo wake wa kukaba, Mbali na nafasi yake ya kiungo mkabaji, pia ana uwezo wa kucheza kama kiungo wa kati pale inapohitajika. Katika msimu wa 2025,26 akiwa na Olympique de Safi, Ngoma alikuwa mchezaji muhimu wa kikosi hicho, akicheza mechi nyingi za ligi na kuonyesha kiwango cha juu cha uthabiti katikati ya uwanja. Kabla ya kutua Morocco, aliwahi kuzichezea klabu mbalimbali barani Afrika na pia amewahi kuitwa katika timu ya taifa ya Congo Brazzaville. Usajili wa Fred Ngoma unaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa Yanga kuimarisha safu ya kiungo kuelekea msimu mpya wa mashindano ya ndani pamoja na michuano ya kimataifa.Ujio wake unatarajiwa kuongeza ushindani mkub...

Yanga na Simba kupigwa New Amaan Stadium

Picha
Mechi ya kuashiria kuanza Ligi Kuu ya NBC Primier League 2026/2027 Ngao ya Jamii inatarajia kuchezwa kwenye uwanja wa New Amaan Stadium mjini Zanzibar. Mechi hiyo iliyopangwa Agosti 12 mwaka huu inayokutanishwa watani wa jadi Yanga na Simba, itachezwa uwanja huo usiku saa 2' 30, Bodi ya Ligi wameelekeza mechi kufanyika Amaan Stadium badala ya uwanja wa Uhuru.

Nyota Yanga ateuliwa Rais wa klabu DR Congo

Picha
Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC, David Molinga 'Falcao' raia wa DR Congo, ameingia kwenye historia mpya katika maisha yake ya soka baada ya kuchaguliwa rasmi kuwa Rais wa Klabu ya AC Bandal kwa mkataba wa miaka mitano.  AC Bandal ni klabu yenye makao yake katika wilaya ya Bandalungwa mjini Kinshasa inayoshiriki Ligi ya EUFKIN-Malebo, na pia ni timu ambayo Molinga mwenyewe aliwahi kuitumikia zamani kama mchezaji. Kupitia ujumbe wake wa shukrani, Molinga amemshukuru Mwenyezi Mungu na kueleza fahari yake kubwa kupewa dhamana ya kuiongoza klabu hiyo iliyowahi kutwaa ubingwa wa Super Coupe ya Kinshasa mwaka 2014.  Amewaahidi wanachama, viongozi na mashabiki kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uwazi ili kuijenga AC Bandal kuwa klabu imara na yenye mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja. Uamuzi huu unamfanya 'Falcao' kujiunga na orodha ya wachezaji wa zamani barani Afrika waliofanikiwa kubadilisha viatu vya soka na kuvaa suti za uongozi katika ngazi ya juu y...

Barker aujia juu uongozi Simba, aponda usajili

Picha
Taarifa zinazoendelea kuzungumzwa ndani ya Simba SC zinaeleza kuwa kocha mkuu Steve Barker hakuwa ameridhishwa na baadhi ya usajili uliofanywa na klabu hiyo kuelekea msimu mpya. Inaelezwa kuwa Barker aliwasilisha mapendekezo yake ya wachezaji aliotaka kuimarisha kikosi, lakini si mapendekezo yote yaliyotekelezwa na uongozi. Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya wachezaji waliosajiliwa hawakuwa sehemu ya chaguo la kwanza la kocha huyo. Majina yanayotajwa ni pamoja na mshambuliaji Doumbia, Chilambo na Jabaar, huku ikielezwa kuwa usajili wao ulifanyika kutokana na maamuzi ya uongozi badala ya mapendekezo ya benchi la ufundi. Aidha, Barker anaripotiwa kushangazwa na kushindwa kwa klabu kukamilisha baadhi ya mahitaji aliyoyaona kuwa ya msingi. Miongoni mwa hoja zinazotajwa ni kushindwa kufanikisha makubaliano yaliyohitaji malipo ya $50,000 kwa Wydad ili kuendelea na mchakato wa kumpata Selemani Gomez, jambo ambalo linaelezwa kuwa lilikuwa sehemu ya vipaumbele vyake katika kuimarisha kikosi...

Zougrana atambulishwa Yanga apewa jezi namba 6

Picha
Klabu ya Yanga SC imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kuimarisha kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano kwa kukamilisha usajili wa kiungo mahiri Mohamed Tchapi Zougrana, ambaye sasa amepatiwa jezi namba 6. Nyota huyu mwenye umri wa miaka 25 na raia wa Burkina Faso amejiunga na Wananchi akitokea MC Alger ya Algeria, baada ya awali pia kuitumikia ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Zougrana anatambulika kwa uwezo wake wa kucheza nafasi ya kiungo wa kati kwa ustadi mkubwa. Ni mchezaji mwenye sifa ya kukaba kwa ufanisi, kumiliki mpira na kuanzisha mashambulizi kwa pasi sahihi. Uwezo huu unamfanya kuwa nyota wa kipekee ambaye anaweza kuimarisha safu ya kiungo ya Yanga SC na kuongeza ubunifu wa kikosi katika mechi ngumu. Jezi namba 6, ambayo mara nyingi huhusishwa na wachezaji wa kiungo wa kati wenye jukumu la kudhibiti mchezo, ni ishara ya imani kubwa ya klabu kwa uwezo wake.

Allan Okello amtaja aliyempeleka Yanga

Picha
Kiungo wa kimataifa wa Uganda, Allan Okello, amefunguka kuhusu mchango wa Dr Lawrence Mulindwa katika safari yake ya kujiunga na Yanga SC, akimtaja kama mtu mwenye nafasi kubwa katika maisha yake. Allan Okello amesema Dr Lawrence Mulindwa ni zaidi ya mshauri kwake, akieleza kuwa anamchukulia kama baba na mlezi aliyekuwa akimuongoza katika hatua mbalimbali za maisha yake ya soka.Okello amesema Mulindwa alimshauri asisite kutumia nafasi ya kuhamia Yanga SC na kumtaka aende Tanzania kuonyesha uwezo wake. Allan Okello: "Dr Lawrence Mulindwa ni kama baba kwangu. Ni mlezi wangu. Aliniambia nitumie fursa hii ya uhamisho kwenda Yanga na nikaitawale Tanzania."Ujumbe huo unaonyesha namna Mulindwa alivyompa Okello moyo na ushauri katika hatua yake ya kuanza sura mpya ya soka nchini Tanzania. # Allan Okello

Ahoua kimeeleweka Jordan

Picha
Mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2024/25, Jean Ahoua ametangazwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Al-Faisaly SC ya Nchini Jordan akitokea klabu ya CR Belouizdad ya Algeria. Nyota huyo wa zamani wa Simba SC, raia wa Ivory Coast, amejiunga na klabu hiyo kwa uhamisho huru baada ya kusitisha mkataba wake na CR Belouizdad kwa makubaliano ya pande zote mbili, akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia miamba hiyo ya Jordanian Pro League. Ahoua 24 alijiunga na Simba SC mnamo Julai 2024 na kuitumikia klabu hiyo Kwa msimu mmoja na nusu ambapo aliisaidia miamba hiyo ya Dar es Salaam kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2025 huku akiwa kinara wa magoli kwenye Ligi kuu bara akifikisha jumla ya magoli 16 kwenye ligi hiyo msimu wa 2024/25. Mnamo Januari 2026 Simba SC alimuuza nyota huyo wa zamani wa Stella Club d'Adjamé ya Nchini kwao Ivory Coast kwenda CR Belouizdad na kuhudumu kwa miamba hiyo ya Algeria kwa nusu msimu.

SAJILI ZA MAJINA MAKUBWA...

Picha
Na Prince Hoza Matua PETER Shalulile ni jina kubwa lililotambulishwa mwanzoni mwa wiki hii ikiwa ni usajili wa klabu ya Yanga SC, huo ni usajili wa nne kati ya maproo waliowasajili msimu huu na kwa mujibu wa viongozi bado wachezaji wakubwa kuwatsngaza. Shalulile ni mchezaji mkubwa barani Afrika, alikuwa anaichezea timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji walioipa jina timu hiyo kutokana na mafanikio yake. Rekodi nzuri ya kufunga hasa kwenye ligi za ndani na kimataifa imemuweka kwenye wakati mzuri kama mchezaji, Shalulile ni mshambuliaji wa kati alikuwa na wastani wa kufunga magoli zaidi ya 20 hivyo aliibuka kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo. Shalulile amewahi kubeba CAF Champions League, pia ameshinda mara kadhaa ubingwa wa nchi hiyo na makombe mengine  ya ndani, ni mmoja kati ya wachezaji wenye sifa kemkem nchini humo. Sidhani kama kuna timu nje ya Afrika Kusini ambayo haina shauku na mchezaji huyo mwenye uraia wa Namibia, Yanga SC...

SAJILI ZA MAJINA MAKUBWA...

Picha
Na Prince Hoza Matua PETER Shalulile ni jina kubwa lililotambulishwa mwanzoni mwa wiki hii ikiwa ni usajili wa klabu ya Yanga SC, huo ni usajili wa nne kati ya maproo waliowasajili msimu huu na kwa mujibu wa viongozi bado wachezaji wakubwa kuwatsngaza. Shalulile ni mchezaji mkubwa barani Afrika, alikuwa anaichezea timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji walioipa jina timu hiyo kutokana na mafanikio yake. Rekodi nzuri ya kufunga hasa kwenye ligi za ndani na kimataifa imemuweka kwenye wakati mzuri kama mchezaji, Shalulile ni mshambuliaji wa kati alikuwa na wastani wa kufunga magoli zaidi ya 20 hivyo aliibuka kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo. Shalulile amewahi kubeba CAF Champions League, pia ameshinda mara kadhaa ubingwa wa nchi hiyo na makombe mengine  ya ndani, ni mmoja kati ya wachezaji wenye sifa kemkem nchini humo. Sidhani kama kuna timu nje ya Afrika Kusini ambayo haina shauku na mchezaji huyo mwenye uraia wa Namibia, Yanga SC...

Simba yatupwa nje Kagame Cup

Picha
Simba SC imehitimisha rasmi safari yake katika michuano ya CECAFA Kagame Cup 2026 baada ya kushindwa kufuzu hatua ya nusu fainali kufuatia matokeo ya michezo ya hatua ya makundi. Baada ya kukusanya pointi mbili pekee katika michezo yake miwili ya kwanza, Simba ilijikuta katika nafasi ngumu ya kusonga mbele. Hata kama itaibuka na ushindi katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Singida Black Stars na kufikisha pointi tano, idadi hiyo haitatosha kuiwezesha kuwa miongoni mwa timu bora zilizomaliza katika nafasi ya pili zitakazofuzu hatua inayofuata. Hali hiyo imechangiwa na matokeo ya makundi mengine, ambapo Al Hilal na Rayon Sports tayari zimekusanya pointi sita kila moja, na hivyo kuondoa uwezekano wa Simba kuingia katika orodha ya timu zitakazofuzu nusu fainali. Kutokana na matokeo hayo, Simba SC inaaga rasmi michuano ya CECAFA Kagame Cup 2026 na sasa itaelekeza nguvu zake katika kujiandaa na msimu mpya wa mashindano ya ndani na kimataifa.

Wydad yamrejesha kundini Seleman Mwalimu "Gomez"

Picha
Selemani Mwalimu yupo jijini Dar Es Salaam akishughulikia safari yake ya kuelekea Morocco kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya. Kocha mpya wa Wydad, Paulo Sergio anataka kuwaona wachezaji wote kambini kabla ya kufanya maamuzi.

Yanga yazima tetesi za Feitoto kutua Yanga'

Picha
Baada ya kuzagaa kwa tetesi zinazomhusisha kiungo wa Azam FC, Feisal Salum, na kujiunga na Yanga, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Kamwe, amesema hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea kati ya pande hizo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kamwe amesema Yanga tayari imekamilisha usajili wa wachezaji wa ndani, hivyo Feisal si sehemu ya mipango ya klabu hiyo. "Feisal Salum ni mchezaji mzuri sana, lakini Yanga SC tumeshafunga usajili wetu wa ndani. Hakuna mazungumzo yoyote kati ya Yanga na Fei/Azam," ameandika Kamwe. Aidha, ameeleza kuwa nafasi mbili za usajili zilizobaki klabuni hapo ni kwa ajili ya wachezaji wa kimataifa pekee.

Al Hilal yaitoa mashindanoni KVZ

Picha
Al Hilal imepata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya KVZ katika mchezo wa mzunguko wa pili wa kundi C la CECAFA Kagame cup 2026. Ushindi huu unawafanya Al Hilal wapande kwenye kilele cha msimamo wa kundi C wakiwa na points zao 6. Mchezo wa kundi C unaofuata hivi punde ni kati ya Rayon Sports dhidi ya Tusker FC.

Arajiga aweka historia Kagame Cup

Picha
Ahmed Arajigga anakua mwamuzi wa kwanza kutoka Tanzania kuchezesha michezo miwili mfululizo ya kombe la CECAFA. Muda huu anasimamia mchezo wa hatua ya makundi kati ya Tusker dhidi ya Rayon Sports. Mashindano hayo yanafanyika ndani ya Rwanda.

Sakata la Seleman Mwalimu lafikia pabaya

Picha
Mshambuliaji wa Simba SC Seleman Mwalimu ameondoka kambini kwa timu hiyo mjini Kigali, Rwanda, na kurejea Dar es Salaam huku hatma yake ndani ya kikosi hicho ikiendelea kujadiliwa. Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Simba unatarajia kuanza mazungumzo na klabu ya Wydad Athletic Club ya Morocco kwa lengo la kufikia makubaliano yatakayomwezesha mshambuliaji huyo kuendelea kuitumikia Simba kwa msimu mmoja zaidi kwa mkopo. Hata hivyo, endapo pande hizo mbili hazitafikia mwafaka, mchezaji huyo atalazimika kurejea Wydad, ambayo bado inamiliki haki za kimkataba za mshambuliaji huyo. Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya jitihada za Simba kuhakikisha inaendelea kuwa na kikosi imara kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Mbegu wa Simba kupaa Czech

Picha
Muda wowote kuanzia sasa kinda wa Simba,Hussein Ally Mbegu (17) atapaa kwenda Czechia ili kufanya majaribio ya wiki mbili na klabu ya Slavia Prague. Simba wametoa ruhusa ya Mchezaji huyo kwenda Czechia ili kujaribu baati yake na kama atafuzu biashara itafanyika. Kwa sasa Mchezaji huyo anahangaikia Viza na muda siyo mrefu ataondoka nchini. Kama biashara hiyo itafanikiwa Simba wataweka kipengele cha “sell-on clause” kama walivyofanya kwa Mbwana Samatta siku za karibuni.

Tuliwazuia Simba- Nahodha Jamus

Picha
Nahodha wa Jamus SC ya Sudan Kusini, Kevin Muhire, amesema walifanikiwa kuizuia Simba kwa kuwabana nyota wake Clatous Chama na Inno Loemba katika mchezo wa Kombe la CECAFA Kagame uliochezwa Kigali, Rwanda. Muhire amesema walitambua ubora wa Simba na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi yaliyolenga kuwazuia viungo hao kutengeneza mashambulizi. "Tulijua Simba ni timu nzuri na ilihitaji pointi tatu, lakini tulifuata mpango wetu na tukapata pointi moja,". Baada ya michezo miwili ya Kundi B, Jamus SC inaongoza kwa pointi nne, Singida Black Stars ina tatu, Simba mbili na Mogadishu City moja. Matumaini ya Simba kutinga nusu fainali sasa yanategemea kuifunga Singida Black Stars katika mchezo wa mwisho wa makundi. Hata hivyo, ushindi pekee unaweza usitoshe, kwani italazimika pia kusubiri matokeo ya mechi kati ya Jamus SC na Mogadishu City ili kujua hatma yake kwenye mashindano

Mayele aaga Pyramids, ahusishwa Simba

Picha
Mshambuliaji Fiston Mayele ameaga rasmi Pyramids FC baada ya kumaliza safari yake ya miaka mitatu ndani ya klabu hiyo. Mayele ameondoka akiwa mchezaji huru, huku akitoa shukrani kwa viongozi, wafanyakazi, wachezaji wenzake na mashabiki wa Pyramids FC kwa imani na sapoti waliompa wakati wote aliokuwa klabuni hapo.Mayele: " Kila stori ina mwisho wake lakini kumbukumbu zinadumu milele. Asante kwa Rais, wafanyakazi, wachezaji wenzangu, mashabiki na kila mmoja aliyekuwa na imani na mimi tangu ujio wangu." Katika kipindi chake Pyramids FC, Mayele amefanikiwa kutwaa mataji manne, akiwemo taji moja la ndani na mataji matatu ya kimataifa. Sasa akiwa mchezaji huru, swali kubwa kwa mashabiki wa soka Tanzania ni kama Simba SC inaweza kuwa moja ya klabu zitakazopigania saini yake Tetesi za usajili wa Mayele zimeanza kuhusishwa na mipango ya Simba ya kufanya usajili mkubwa kuelekea msimu mpya, hasa baada ya Yanga SC kuendelea kuimarisha kikosi chake kwa usajili wa nyota mbalimbali.Hata hiv...

Ben Lee atua Tanzania

Picha
Tanzania imepiga hatua nyingine katika juhudi za kuendeleza mchezo wa uogeleaji kufuatia kuwasili kwa kocha wa kimataifa, Ben Lee, ambaye atatoa mafunzo ya kiwango cha kimataifa kwa waogeleaji, makocha na wazazi. Mafunzo hayo yatafanyika kupitia programu maalumu iliyoandaliwa na Monti International School. Ujio wa Ben Lee unaelezwa kuwa ni hatua muhimu katika safari ya kuinua viwango vya uogeleaji nchini kwa kuwaletea Watanzania utaalamu wa kimataifa bila kulazimika kusafiri nje ya nchi. Kocha huyo ana uzoefu mkubwa wa kuwafundisha waogeleaji walioshiriki mashindano ya NCAA na Olimpiki. Akizungumza na waandishi wa habari katika mapokezi ya kocha huyo jijini Dar es Salaam, Afisa Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Petro Gallos mbali na kupongeza ujio wake, amesema wakufunzi wa ndani wa mchezo huo wanapaswa kutumia mwanya huo adhimu kwa kuchota ujuzi wenye manufaa.

Neo Maema arejea Mamelodi

Picha
Kiungo mshambuliaji mwenye uraia wa Afrika Kusini, Neo Maema ambaye mkataba wake na Simba umemalizika rasmi, hatimaye amerejea Mamelodi Sundowns. Taarifa zenye uhakika ambazo Mambo Uwanjani Blog imeyhibitisha kwamba mchezaji huyo amerejea timu yake ya nyumbani. Kipengere cha mkataba wake na Mamelodi dhidi ya Simba kimemfanya arejee tena, Maema amekuwa na kiwango kizuri msimu uliopita na kupelekea Mamelodi kumuhitahi tena.

Simba yanogewa na sare

Picha
Timu ya Simba ya Tanzania imeendelea kulazimishwa sare 0-0 tasa katika michuano ya kombe la Kagame Cup nchini Rwanda dhidi ya Jamus ya Sudan Kusini na kufanya nafasi yake ya kusonga kuwa ngumu. Sasa italazimika kushinda dhidi ya Singida Black Stars watakaocheza mchezo wa mwisho ama sivyo itatolewa, jioni hii Singida Black Stars imeichapa Mogadishu City Club mabao 4-1 na kuweka hai nafasi yake ya kutetea kombe hilo. Simba sasa ina pointi mbili baada ya sare mbili wakati Singida Black Stars wana pointi tatu na wanashika nafasi ya pili wakati Jamus vinara wa kundi.

Sio kweli Injinia Hersi kamsajili Shalulile ashinde uchaguzi

Picha
Kwamba Eng Hersi Said @caamil_88 alihitaji kumsajili Peter Shalulile ili ashinde uchaguzi? Sio kweli... Hakuna mwana Yanga ambaye ana mashaka na Hersi na GSM, wamebeba ubingwa mara 5, wamemfunga Simba mara nyingi kwenye kipindi chao, wamefika fainali ya CAFCC. N arudia, Hersi hana wasiwasi wa kushinda uchaguzi wa Yanga na hahitaji nguvu kubwa kurejea madarakani. Turudi kwa Shasha Man (Peter Shalulile) Nimesikia kwamba Simba walimtaka Shalulile lakini wakajiondoa baada ya kushauriwa na Steve Barker kwa hoja hizi 3:- 1) Umri wa mchezaji 2) Kiwango cha mchezaji 3) Fedha anayotaka Kwamba Kocha Steve Barker alishauri kuwa umri wa miaka 32 na kiwango chake cha hivi karibuni (current form) haviendani na fedha anayoitaka mchezaji na wakala wake (Usd 750k kwa mwaka) Kwamba Shalulile msimu uliopita kafunga mabao matatu katika mechi 13 (moja la penati) hivyo uwezo wake umepungua... Kwa mtazamo wangu, Nafikiri tunaposema kuhusu umri wa Peter tusisahau kwamba Meddie Kagere akiwa na miaka 32 alifung...

Ally Kamwe aanika viingilio Wiki ya Wananchi

Picha
Klabu ya Yanga SC imetangaza rasmi viingilio vya Wiki ya Wananchi Agosti 9 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Akizungumza na vyombo vya habari, Afisa Habari wa klabu hiyo Ally Kamwe amesema kuwa ili kushuhudia uzinduzi wa kikosi chao nyota wapya na burudani ya kipekee itaoneshwa kwa shilingi 300, 000. Jezi mpya ya msimu iliyosainiwa na mchezaji unayemchagua. usafiri wa kwenda na kurudi uwanjani kutoka Serena Hotel. chakula wakati wa mapumziko uwanjani 𝐕𝐈𝐏 𝐓𝐢𝐜𝐤𝐞𝐭 – 𝐓𝐒𝐡 𝟏𝟎𝟎,𝟎𝟎𝟎 M𝐳𝐮𝐧𝐠𝐮𝐤𝐨 – 𝐓𝐒𝐡 𝟐𝟎,𝟎𝟎𝟎 Nafasi ni chache sana Uwanja wa Uhuru, wahi mapema kukata tiketi yako.

Rais Samia aipongeza Twiga Stars

Picha
Ninaipongeza Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars), kwa kuanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 nchini Morocco kwa ushindi dhidi ya Timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini, (Banyana Banyana). Ninaungana na Watanzania wote kuitakia kila la kheri Twiga Stars inapoendelea kupeperusha bendera ya Taifa letu katika michezo inayofuata. Endeleeni kupambana kwa moyo huo huo, mkionesha uzalendo, nidhamu na ari ya ushindani inayolitangaza vyema Taifa letu.

Peter Shalulile asajiliwa na Yanga

Picha
Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Namibia, Peter Shalulile, aliyekuwa akiitumikia Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Shalulile anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Yanga kama sehemu ya maboresho makubwa ya kuelekea msimu mpya, huku akitajwa kuziba pengo lililoachwa na mshambuliaji Prince Dube, ambaye ameondoka ndani ya klabu hiyo.

Mtoto wa kaka wa Diamond Platinum apewa jina la Aaliyah

Picha
Ricardo Momo ambaye ni kaka wa Diamond Platnumz amethibithisha kuwa mtoto wake aliyozaliwa amepewa jina la Aaliyaah. Riacardo Momo ameeleza kuwa jina hilo alikuwa nalo tangu kipindi cha nyuma kwasababu huwaga anaplan za majina kabla hajapata watoto. Aidha Ricardo Momo amesema kuwa haoni ubaya kwenye jina la Aaliyaah licha ya jina hilo kufanana na Aaliyaah wa Wasafi. ''Mimi huwaga na plan za majina kabla ya kupata watoto''Amesema -Ricardo

Feitoto' kurudi Yanga

Picha
Klabu ya Young Africans SC (Yanga SC) imeendelea kuibua mijadala mikubwa katika anga za soka la Tanzania baada ya kuhusishwa na mpango wa kumrejesha kiungo mshambuliaji wao wa zamani, Feisal Salum maarufu kama Feitoto, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Azam FC. Hatua hii imeibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wa Wananchi, kwani Feisal ni mchezaji mwenye historia kubwa na mchango wa kipekee katika mafanikio ya Yanga SC kabla ya kuondoka. Feisal anatambulika kama kiungo mwenye ubunifu, kasi na uwezo wa kutengeneza nafasi za mabao. Ni mchezaji ambaye mara nyingi huleta uwiano wa kiufundi na kuongeza chaguo la ushambuliaji kwa benchi la Yanga SC. Uwezo wake wa kupenya safu za ulinzi za wapinzani na kutoa pasi sahihi unamfanya kuwa mchezaji wa thamani kubwa kwa kikosi chochote. Hii ndiyo sababu mashabiki wengi wa Yanga SC wanatamani kumuona akirejea Jangwani ili kuimarisha safu ya kiungo na kuongeza nguvu katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Girumugisha aikwepa Yanga na kutimkia Libya

Picha
Winga Jean Claude Girumugisha amewasili nchini Libya kwaajili ya kukamilisha mchakato wake wa usajili wa kujiunga na Al Ahli Tripoli akitokeaAl Hilal Omdurman kwa msimu mpya! Jean Claude Girumugisha hatajiunga na Young Africans SC kuelekea msimu ujao wa 2026-27 ambao waliulizia thamani ya winga huyo na hawakurudi tena mezani kupambania saini na huduma ya mchezaji huyo ambaye amekuwa na misimu bora sana

Bajaber na Simba kwishinei

Picha
Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano rasmi ya kuvunja mkataba na kiungo mshambuliaji raia wa Kenya, Mohamed Bajaber (23). ​Uamuzi huo umekuja baada ya mchezaji huyo kuonekana kutokuwa kwenye mipango ya kocha mkuu wa Msimbazi, Steve Barker, jambo lililopelekea pande zote mbili kuridhia kutengana kwa amani. Bajaber tayari ameanza mchakato wa kutafuta changamoto mpya katika klabu nyingine.

Al Ahly yaangukia Shirikisho

Picha
Maamuzi ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kukataa ombi la Shirikisho la Soka la Misri (EFA) la kuongeza idadi ya timu kwenye Ligi ya Mabingwa, yamekuja kufuatia klabu kongwe ya Al Ahly kumaliza katika nafasi inayowatupa nje ya kufuzu CAF Champions League kwa msimu wa 2026/27. ​Kulingana na msimamo wa Ligi Kuu ya Misri, Al Ahly imeshindwa kukamata nafasi mbili za juu zinazotoa tiketi ya Ligi ya Mabingwa, na badala yake itabidi washiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup). ​Jaribio la EFA kutaka kuokoa jahazi la miamba hiyo ya Cairo kwa kuomba nafasi zaidi kutoka CAF limegonga mwamba, ikimaanisha mabingwa hao mara nyingi zaidi wa Afrika watapaswa kupambana kwenye Kombe la Shirikisho msimu ujao.

Makamu wa Rais Yanga awatoa hofu kuhusu uwanja Jangwani

Picha
Makamu wa Rais wa klabu ya Young Africans (Yanga SC), Arafat Haji, amewatoa hofu mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuhusu mradi wa ujenzi wa uwanja wao wa kisasa eneo la Jangwani, kwa kueleza kuwa tayari wameshasaini mkataba rasmi na mwekezaji GSM tangu tarehe 12 na mchakato wa maandalizi unaendelea vizuri. Ametoa ufafanuzi kuwa sababu ya kutooana ujenzi wa moja kwa moja ukiendelea eneo la tukio ni kutokana na kuwepo kwa miradi mingine inayotegemeana kama mradi wa Mto Msimbazi na daraja jipya, huku vifaa vya uwanja huo vikiwa vinaandaliwa na kuunganishwa huko vinakotoka. Arafat aliongeza kuwa uwanja huo utatumia teknolojia ya kisasa na hautakuwa wa zege tupu, bali vifaa vingi vitaletwa kutoka nje ya nchi na kuunganishwa mahali hapo baada ya kukamilisha kujaza eneo hilo ili kufikia kiwango na urefu ulioshauriwa na wataalamu wa Bonde la Jangwani. Hatua hiyo inachukuliwa kwa umakini mkubwa ili kuepuka changamoto za mafuriko na athari za maji ya mvua, huku wakihakikisha ujenzi unafuata ...

Omari Omari rasmi Singida Black Stars

Picha
Singida Black Stars FC imekamilisha usajili wa kiungo Omary Omary kutoka Mashujaa FC ambayo anaitumikia kwa mkopo akitokea Simba SC. Omary Jr alikuwa na mkataba wa miaka mitatu na Simba SC na mpaka sasa Singida Black Stars ilishamalizana na Simba SC kwa uhamisho huo kwa kila kitu!

Dkt Nchinbi atembelea uwanja wa Samia Arusha

Picha
Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Arusha, utakaotumika katika fainali za AFCON 2027, unaojengwa jijini Arusha. Dkt. Nchimbi amepongeza maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo, ambapo amesema ni faraja kuona ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa ili kuvutia michuano hiyo kufanyika nchini Tanzania, inatakelezwa kikamilifu. Makamu wa Rais amemshukuru Rais kwa kuendelea kutoa fedha ili kuhakikisha uwanja huo unakamilika kwa wakati. Dkt. Nchimbi ameishukuru Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na mkoa wa Arusha, wakandarasi na mshauri Elekezi kwa kazi waliyofanya katika Uwanja huo. Makamu wa Rais amewataka viongozi wa wizara pamoja na Mkoa wa Arusha kusimamia vema agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha barabara zinazotumika katika kufika uwanjani hapo zinakamilika kwa wakati.

Kagere amkosoa Ibrahim Doumbia

Picha
Aliyekuwa mshambuliaji hatari wa Simba SC na timu ya taifa ya Rwanda, Medie Kagere, amefunguka na kueleza kusikitishwa kwake na nafasi ya goli aliyokosa mshambuliaji mpya wa Wekundu wa Msimbazi, Ibrahim Doumbia raia wa Mali. ​Akizungumzia tukio hilo lililokea katika mchezo wao wa CECAFA Kagame Cup, Kagere amesema: ​🗣️ "Kwangu binafsi, ile naichukulia kama ni nafasi ya dhahabu kwa mshambuliaji. Sijui ni kwa nini alichagua kufunga kwa namna ile; angechagua namna nzuri ya kufunga, lingekuwa ni goli rahisi." ​Unadhani Doumbia alikosa umakini au presha ya mechi za mwanzo imemshika ndani ya Simba SC? Dondosha maoni yako!

Bodi ya Ligi kuanzisha sheria mpya kwa wachezaji wa kigeni

Picha
Bodi ya Ligi Tanzania inatarajiwa kuanzisha kanuni mpya ya usajili wa wachezaji wa kigeni itakayoanza kutumika kuanzia msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya NBC. Kwa mujibu wa kanuni hiyo mpya, mchezaji wa kigeni atakayehitaji kusajiliwa na klabu yoyote ya Ligi Kuu ya NBC atalazimika kuwa ameiwakilisha nchi yake katika timu ya taifa ya U-17, U-20 au timu ya taifa ya wakubwa, kuanzia mwaka 2024 na kuendelea, ili aweze kustahili kusajiliwa. Hata hivyo, sheria hiyo haitawahusu wachezaji wa kigeni ambao tayari walikuwa wakicheza Ligi Kuu ya NBC katika msimu wa 2025/26 au misimu iliyotangulia. Hivyo, wachezaji hao wataendelea kustahili kucheza bila kulazimika kutimiza sharti hilo jipya.

Libasse Gueye anauzwa

Picha
Klabu ya Simba SC inadaiwa kupokea ofa mbili kutoka nje ya Tanzania kwa ajili ya winga wake wa Senegal, Libasse Gueye.OFA ya kwanza imetoka kwa klabu ya Morocco yenye thamani ya $500,000 (takribani Sh bilioni 1.3), wakati ofa ya pili kutoka klabu ya Qatar inatajwa kuwa na thamani ya $700,000 (takribani Sh bilioni 1.8). Hata hivyo, Simba inadaiwa kuwa tayari kumuuza nyota huyo endapo italetewa ofa ya $1,000,000 (takribani Sh bilioni 2.6).Endapo Libasse Gueye ataondoka Msimbazi, Simba inatarajiwa kuelekeza nguvu zake kwenye usajili wa winga mwingine wa kigeni ili kuziba nafasi yake katika kikosi.

Seleman Mwalimu Simba haina mamlaka ya kumtumia

Picha
Klabu ya Simba SC bado haina mamlaka ya kumtumia mshambuliaji Seleman Mwalimu Kwenye mchezo wowote ule bila idhini ya klabu yake mama ya Wydad AC, Katika mchezo wa leo wa CECAFA KAGAME CUP dhidi ya klab ya Mogadishu City Club Seleman Mwalimu hakujumuishwa, Klab ya Simba inapambana kuhakikisha inampata mshambuliaji huyo kwa mkataba wa mkopo kama ilivyokuwa hapo awali,