Allan Okello amtaja aliyempeleka Yanga

Kiungo wa kimataifa wa Uganda, Allan Okello, amefunguka kuhusu mchango wa Dr Lawrence Mulindwa katika safari yake ya kujiunga na Yanga SC, akimtaja kama mtu mwenye nafasi kubwa katika maisha yake.

Allan Okello amesema Dr Lawrence Mulindwa ni zaidi ya mshauri kwake, akieleza kuwa anamchukulia kama baba na mlezi aliyekuwa akimuongoza katika hatua mbalimbali za maisha yake ya soka.Okello amesema Mulindwa alimshauri asisite kutumia nafasi ya kuhamia Yanga SC na kumtaka aende Tanzania kuonyesha uwezo wake.

Allan Okello: "Dr Lawrence Mulindwa ni kama baba kwangu. Ni mlezi wangu. Aliniambia nitumie fursa hii ya uhamisho kwenda Yanga na nikaitawale Tanzania."Ujumbe huo unaonyesha namna Mulindwa alivyompa Okello moyo na ushauri katika hatua yake ya kuanza sura mpya ya soka nchini Tanzania. #

Allan Okello

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI