Simba yanogewa na sare
Timu ya Simba ya Tanzania imeendelea kulazimishwa sare 0-0 tasa katika michuano ya kombe la Kagame Cup nchini Rwanda dhidi ya Jamus ya Sudan Kusini na kufanya nafasi yake ya kusonga kuwa ngumu.
Sasa italazimika kushinda dhidi ya Singida Black Stars watakaocheza mchezo wa mwisho ama sivyo itatolewa, jioni hii Singida Black Stars imeichapa Mogadishu City Club mabao 4-1 na kuweka hai nafasi yake ya kutetea kombe hilo.
Simba sasa ina pointi mbili baada ya sare mbili wakati Singida Black Stars wana pointi tatu na wanashika nafasi ya pili wakati Jamus vinara wa kundi.
