Al Ahly yaangukia Shirikisho
Maamuzi ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kukataa ombi la Shirikisho la Soka la Misri (EFA) la kuongeza idadi ya timu kwenye Ligi ya Mabingwa, yamekuja kufuatia klabu kongwe ya Al Ahly kumaliza katika nafasi inayowatupa nje ya kufuzu CAF Champions League kwa msimu wa 2026/27.
Kulingana na msimamo wa Ligi Kuu ya Misri, Al Ahly imeshindwa kukamata nafasi mbili za juu zinazotoa tiketi ya Ligi ya Mabingwa, na badala yake itabidi washiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup).
Jaribio la EFA kutaka kuokoa jahazi la miamba hiyo ya Cairo kwa kuomba nafasi zaidi kutoka CAF limegonga mwamba, ikimaanisha mabingwa hao mara nyingi zaidi wa Afrika watapaswa kupambana kwenye Kombe la Shirikisho msimu ujao.
