Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2026

Hatuna habari na Fadlu- AliKamwe

Picha
Klabu ya Young Africans SC kupitia kwa Afisa Habari wake, Ally Kamwe, imetolea ufafanuzi wa haraka uvumi unaoendelea mitandaoni kuhusu mchakato wa kusaka kocha mpya. Kamwe ameweka wazi kuwa uongozi haujafanya mazungumzo yoyote na kocha Fadlu Davids na kuwataka mashabiki kupuuza taarifa zote za usajili zinazosambazwa kwa sasa, kwani nguvu zao zote zimeelekezwa kwenye mchezo wa kesho wa kusaka ubingwa. ​Ujumbe wake kamili unasomeka hivi:​"Uongozi wa YANGA SC haujafanya mazungumzo Yoyote wala hauna mpango wa kumuajiri Kocha Fadlu Davis .. ​Ni vile tu watu wanapitia kipindi kigumu kupata Breaking News za YANGA ndio maana wanaanzisha jambo la kulimaliza wenyewe juu kwa juu ​Kwenu Wananchi, Habari sahihi za YANGA SC mtazipata kupitia YANGA APP na Kurasa zetu za Mitandao ya Kijamii za klabu ya YANGA ​Kipindi hiki, Habari yoyote ya Usajili wa Wachezaji au Kocha utakaousoma huku Mitandaoni, Ni UZUSHI na UONGO. ​Kwa sasa, Focus yetu Yote iko kesho. Twendeni Uwanjani Tukapambanie UBINGWA wet...

Rais Samia aipongeza Yanga kutwaa ubingwa

Picha
Ninaipongeza Klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo. Mafanikio haya ni ushahidi wa juhudi, nidhamu na kujituma kwa wachezaji, benchi la ufundi, uongozi pamoja na mashabiki. Aidha, ninazipongeza klabu zote zilizoshiriki Ligi Kuu msimu huu kwa ushindani mzuri uliofanya mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania kuendelea kukua, kuvutia na kuongeza hamasa kwa mashabiki pamoja na wadau wa mchezo huu.

Mangungu afunguka baada ya kukosa ubingwa

Picha
Niwaambie tu kuwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu huu amepatikana kwa kupendelewa na kila mtu anajua na Waandishi mnaelewa.. hakuna fair competition na makosa ya kibinadamu yalikuwa ya kutosha kwa marefa waliochezesha mechi za Bingwa (Yanga) ". - Mwenyekiti wa Simba akiongea baada ya mchezo wa Simba SC dhidi ya KMC kumalizika.. akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Young Africans SC kuwa Bingwa wa Ligi kuu msimu huu.

Yanga bingwa Ligi Kuu bara, yarudia historia ya mwaka 1968-1972

Picha
TIMU ya Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam. Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Mpumelelo Dube dakika ya nane, kiungo Maxi Mpia Nzengeli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mshambuliaji Laurindo Dilson Maria AurĂ©lio ‘Depu’ kutoka Angola dakika ya 66. Kwa ushindi huo, Yanga SC inamaliza Ligi Kuu msimu wa 2025 – 2026 ikiwa na pointi 75, mbili Zaidi ya watani wao, Simba SC waliomaliza nafasi ya pili baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, KMC FC jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Hilo linakuwa taji la tano mfululizo la Ligi Kuu kwa Yanga kuanzia msimu wa 2021–2022, 2022–2023, 2023–2024 na 2024–2025 na hiyo inakuwa mara ya pili kwa wana Jangwani hao kutwaa mataji ya Ligi Kuu mara tano mfululizo baada ya kufanya hivyo misimu ya 1968, 1969, 1970, 1971 na 1972. Kwa u...

Raja Casablanca yanasa kiungo wa Yanga

Picha
Klabu ya Raja Casablanca inafikiria kumrudisha kiungo wao Moussa Balla Conte katika klabu yake ya Young Africans SC baada ya kuwatumikia kwa mkopo! Raja AC hawaridhishwi na kiwango chake na atakutana na Fadlu Davids ikiwa atamalizana na Young Africans SC kwa makubaliano ya mwisho pia Raja AC wanatarajia kuwasiliana na Young Africans SC ili kuwapa taarifa kuwa hawatamuongezea mkataba wa muda mrefu kiungo huyo.

Ajitokeza kugombea na Injinia, Yanga

Picha
Mfanyabiashara mkubwa nchini katika sekta ya simu, Zahoro Matelephone, ameripotiwa kuchukua fomu katika makao makuu ya Klabu ya Yanga kwa ajili ya kuwania nafasi ya ujumbe kwenye uongozi wa klabu hiyo. Hatua hiyo inaongeza ushindani katika mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Yanga, huku wadau na mashabiki wakifuatilia kwa karibu majina yanayojitokeza kuwania nafasi mbalimbali. Iwapo atafanikiwa kuchaguliwa, Zahoro atakuwa sehemu ya uongozi utakaosimamia maendeleo ya klabu kuelekea misimu ijayo.

Top scorer wa Simba Queens atimka

Picha
Mshambuliaji wa Simba Queens, Jetrix Shikangwa, ameondoka rasmi klabuni hapo na kujiunga na FC Masar ya Misri. Jetrix anaondoka baada ya msimu bora, akifunga mabao 16 na kuwa mmoja wa nyota walioisaidia Simba Queens kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania. Anatarajiwa kuungana na Mtanzania, Hasnath Ubamba, anayekipiga FC Masar.

Seleman Mwalimu atabaki Simba

Picha
Kocha Steve Barker amemtaja Selemani Mwalimu kuwa mmoja wa washambuliaji anaotaka kubaki nao Simba SC kuelekea msimu wa 2026/27 Mkataba wa sasa wa mkopo wa Selemani Mwalimu na Simba SC hauna kipengele chochote cha kuongeza muda wa mkopo au kumnunua moja kwa moja Hii ina maana kuwa Mwalimu anatakiwa kurejea Wydad AC mara baada ya mkopo wake kumalizika, then Simba SC na Wydad AC wafungue mazungumzo mapya(kama wanahitaji kubaki naye) Taarifa zinaeleza kuwa Wydad AC wako tayari kumruhusu Mwalimu aondoke kwa uhamisho wa moja kwa moja(kuuzwa), na si kwa mkopo mwingine Hata hivyo, ada inayotarajiwa kuhitajika inaweza kuwa changamoto kwa Simba SC Licha ya kuvutiwa na vilabu kadhaa, Selemani Mwalimu ameipa Simba SC kipaumbele na yuko tayari kusubiri uamuzi wa Simba sc kabla ya kusikiliza ofa nyingine Kwa sasa, mchezaji anaitaka Simba kwanza... lakini uamuzi wa mwisho utategemea kama Simba SC na Wydad AC watafikiana

Barker amng' ang' ania Ibraheem Jabaar

Picha
Kocha mkuu wa Simba Steve Barker,ana-push sana Simba wakamilishe usajili wa kiungo wa Stellenbosch raia wa Nigeria, Ibraheem Jabaar (23). Personal terms Siyo ishu kwani mchezaji huyo yuko huru. Kocha anamtaka Jaabar kwani anamfahamu vizuri ila viongozi wa Simba wanamtaka namba 10 wa Chile,Diego Mauricio ambae nae ni mchezaji huru. Simba wanamuona Diego ni Top Top Number 10 ambae atakuju kumpa changamoto Chota Chama….na Simba wako tayari kumlipa mshahara wa $20,000 (52,646,460) kila mwezi. Wiki ijayo itakuwa muhimu sana kufanya maamuzi ya nani aje kati ya Diego Mauricio au Jabaar.

Azam FC yamkomalia Iddi Nado kwenda Yanga

Picha
Azam FC imeanza mazungumzo na kiungo wake Nado kwa lengo la kuongeza mkataba wake, kufuatia kiwango bora alichoonyesha tangu aliporejea kikosini mwezi Julai 2025. Nado, ambaye alijiunga na Azam FC mwaka 2019 akitokea Mbeya City, ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya kikosi hicho kutokana na mchango wake mkubwa katika safu ya kiungo. Taarifa zinaeleza kuwa hatua ya Azam FC kumuita mezani inalenga kuhakikisha inamdumisha nyota huyo, hasa baada ya kuvutia macho ya watani wa jadi, Yanga SC na Simba SC, ambao wanatajwa kuwa na nia ya kupata saini yake. Hatma ya Nado sasa inategemewa kuamuliwa na mazungumzo kati yake na Azam FC huku dirisha la usajili likiendelea kushika kasi. 

Rasmi, Yanga wanamleta Fadlu

Picha
Inaripotiwa nchini Afrika Kusini mchana huu kwamba, Yanga Afrika wameweka ofa mezani na wako kwenye mazungumzo kumsaini Kocha Fadlu Davids kama kocha wake mpya mkuu kuelekea msimu ujao. Fadlu Davids aliitumikia Simba Sports msimu huu, hapa Tanzania kabla ya kutimkia Raja Club huko Morocco ambako baada ya matokeo mabovu dhdi ya vilabu vikubwa na kuukosa Ubingwa wa Botola Pro alifutwa kazi jijjni Casablanca wiki chache zilizopita.

Diarra kinara wa clean sheets

Picha
Kipa wa Yanga SC na Timu ya Taifa ya Mali, Djigui Diarra, ameendelea kuonyesha kiwango cha juu baada ya kufikisha clean sheets 17 kufuatia mchezo dhidi ya TRA. Rekodi hiyo inamfanya kuwa kipa mwenye clean sheets nyingi zaidi msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku kukiwa bado kumesalia mchezo mmoja kabla ya msimu kumalizika. Hii ni mara ya tatu kwa Djigui Diarra kumaliza akiwa kinara wa clean sheets tangu ajiunge na Yanga SC, jambo linaloonyesha uthabiti wake langoni kwa misimu kadhaa mfululizo. Rekodi zake za Clean Sheets: 2021/22 – 15 2022/23 – 17 2023/24 – Ley Matampi (15) 2024/25 – Moussa Camara (19) 2025/26 – 17 (bado mchezo mmoja umebaki) Djigui sasa ana nafasi ya kuongeza idadi hiyo katika mchezo wa mwisho wa msimu na kuendelea kuimarisha rekodi yake kama mmoja wa makipa bora kuwahi kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara.

TZ Prisons, Mbeya City na Mtibwa Sugar hatarini kushuka daraja

Picha
TIMU za Mbeya City na Tanzania Prisons zote za Mbeya – kwa pamoja na Mtibwa Sugar ya Morogoro zote zipo hatarini kushuka Daraja baada ya mechi za mzunguko wa 29 leo. Wakiwa nyumbani, Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, huku Mbeya City ikitoa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Dodoma Jiji FC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Baada ya matokeo hayo, Mtibwa Sugar inashukia nafasi ya 15 ikibaki na pointi zake 27, nyuma ya Tanzania Prisons nafasi ya 14 na Mbeya City nafasi ya 13 baada ya timu hizo zote kucheza mechi 29 zikiwa hatarini kuungana na KMC FC ambayo tayari imeshuka daraja. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, mabingwa watetezi, Yanga SC wamelikaribia taji la tano mfululizo la Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Nao Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es ...

Azam FC yailaza Coastal Union 2-0

Picha
TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Mabao ya Azam FC yamefungwa na beki Muivory Coast, Landry Ahoutou Angenor Zouzou dakika ya pili na kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 32 hilo likiwa bao lake la 15 la msimu na kuendelea kuongoza mbio za ufungaji Bora. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 61, ingawa inabaki nafasi ya pili, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 33 nafasi ya tisa kufuatia timu hizo nazo kucheza mechi 29 pia.

Simba haijaisha mpaka iishe

Picha
VIGOGO Simba SC, wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC yamefungwa na mawinga, Elie Mpanzu Kibisawala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (drc) dakika ya 28 na Alain Anicet Oura kutoka Ivory Coast dakika ya 59. Kwa ushindi huo, Simba SC wanafikisha pointi 70, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga SC kufuatia timu zote kucheza mechi 29 kuelekea mechi za mwisho za msimu Jumanne. Kwa upande wao Singida Black Stars baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 50 kufuatia kucheza mechi 29 pia wakisalia pia katika nafasi ya nne.

Yanga yakaribia taji la tano Ligi Kuu bara mfululizo

Picha
MABINGWA watetezi, Yanga SC wamelikaribia taji la tano mfululizo la Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Shujaa wa Yanga SC leo ni winga Mganda, Allan Jolly Okello ‘Star Boy’ aliyefunga mabao yote hayo matatu peke yake dakika za 27, 51 kwa penalti na 57. Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 72 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili Zaidi ya wapinzani wao, Simba SC kufuatia timu zote kucheza mechi 29 kuelekea mechi za mwisho za msimu Jumanne. Kwa upande wao, TRA United baada ya kupoteza mchezo wa leo inabaki na pointi zake 42 kufuatia kucheza mechi 29 pia wakisalia pia katika nafasi ya tano.

Tumepanga kuwashambulia Yanga- Ndayiragije

Picha
Kocha Mkuu wa TRA United SC, Etienne Ndayiragije, ameweka wazi kuwa mchezo wao ujao dhidi ya mabingwa watetezi, Young Africans SC, utakuwa ni fursa adhimu ya kuendelea kuitangaza na kuitambulisha timu yao kwa Watanzania. Ndayiragije amebainisha kuwa tofauti na mechi ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa kwenye uwanja wao wa nyumbani jijini Arusha na kumalizika kwa sare ya 0-0, mchezo wa kesho utakuwa wa aina yake kwani unachezwa katika Uwanja wa KMC huku kikosi chake kikiwa kimeshapata mdundo mzuri wa ushindani. Katika upande wa mbinu, kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa amefunguka mpango madhubuti wa kukabiliana na safu kali ya ushambuliaji ya Yanga SC, akisisitiza kuwa hawatenda kuzuia badala yake wataingia kwa kushambulia zaidi ili kuwalazimisha wapinzani wao kurudi nyuma kulinda lango lao. Aidha, Etienne Ndayiragije amepiga chini dhana kuwa timu hiyo ni tishio wakiwa tu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, akitolea mfano matokeo yao makubwa ya ugenini ikiwemo ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Si...

Nasri Kombo mali ya Yanga msimu ujao

Picha
Yanga SC wapo hatua za mwisho kukamilisha dili hili beki wa kati bwana mdogo Nasri Kombo ambaye amekuwa na kiwango bora msimu huu ndani ya TRA United. Yanga SC inataka beki mzawa wa kwenda kuongeza nguvu kwenye ukuta wao pamoja na kutoa Challange kwa Job,Bacca na Mwamnyeto.

Kitambala awaniwa na Singida Black Stars

Picha
Singida Black Stars,wako kwenye mazungumzo ya kina na mshambuliaji wa Azam FC,Jephte Kitambala (27). Mazungumzo yako kwenye hatua nzuri na Kitambala ameonyesha nia ya kujiunga na Singida mwishoni mwa msimu huu.

Barker aeleza mambo matano kuelekea mechi ya kesho

Picha
Mambo 5 Aliyoyasema Kocha Steve Barker Kuelekea Mechi ya Kesho Dhidi ya Singida Black Stars: (LIGI KUU). Tahadhari kwa Mossi Ndumumwe: Barker amekiri kuwa safu ya ushambuliaji ya SBS ni hatari, na Kinarabwa mabao Mossi Ndumumwe amekuwa na moto mkali tangu Januari. Ni mtu wa kuchungwa kwa ukaribu sana. Matumaini ya Ubingwa: Simba bado hawajakata tamaa. Hesabu ni kushinda mechi zao zote huku wakivizia wapinzani wao kuteleza na kudondosha pointi. Vita ya Mbinu: Kocha anaamini wachezaji wake wamekomaa zaidi kimbinu kuliko wapinzani wao, hivyo ushindi kesho ni amri! Ripoti ya Kikosi: Kibabage bado yuko mashakani kuanza hali yake (itaendelea kuangaliwa leo), Anicet Oura kuna uwezekano mkubwa akaanza, na habari njema ni kurejea kwa Morice Abraham kutoka majeraha. Nguvu ya Mashabiki: Barker amewapongeza Wanasimba kwa support ya maana tangu ameanza kazi Msimbazi, na anaomba mzigo uendelee kesho.

Kiboko ya Yanga, atua Caps United Zimbabwe

Picha
Uchizi Vunga amejiunga na klabu ya CAPS United inayoshiriki Ligi Kuu ya Zimbabwe akitokea Silver Strikers FC. - Vunga anakuwa mchezaji wa pili kuondoka katika wiki za hivi karibuni, kufuatia kuondoka kwa beki wa kulia McDonald Lameck ambaye amejiunga na Hard Rock FC. - Vunga alijiunga na Silver Strikers mwaka 2021 akitokea Mzuzu City Hammers, iliyokuwa ikijulikana awali kama Ekwendeni Hammers

Tuzo ya MVP yamponyoka Feitoto

Picha
Inawezekana ubora wa Feisal Salum Feitoto' usitoshe pekee kumbeba kwenye mbio za tuzo ya mchezaji bora wa msimu (MVP) ikiwa hana ubingwa wa Ligi Kuu mkononi. Mambo yamebadilika kwenye takwimu: Asisti: Elie Mpanzu sasa ndiye kinara akiwa nazo 9, akimwacha Fei Toto mwenye 8. Ufungaji: Yupo sawa na Mossi Ndumumwe, wote wakiwa na mabao 14, Allan Okello hayupo mbali (11). Bila kombe la Ligi Kuu, njia pekee ya Fei kutwaa tuzo ya MVP inakuwa ni kutawala takwimu zote mbili. Mchezo wa jana dhidi ya Yanga SC unaweza ukawa umehamisha mjadala mzima kwenda kwa wachezaji wa Simba au Yanga (iwapo mmoja wapo akibeba ubingwa), labda tu kama Feisal atarejesha ufalme wake kileleni kwenye takwimu. Haina ubishi, Fei Toto ni kiungo mfungaji bora zaidi nchini tangu atue Chamazi, lakini mechi dhidi ya Coastal Union na Dodoma Jiji ndizo zitakazoamua hatma yake.

Aucho akaribia kutua Gor Mahia

Picha
Nahodha wa Uganda Cranes, Khalid Aucho, anatajwa kuwaniwa na klabu za Gor Mahia na Tusker FC kwa ajili ya usajili wake, kwa mujibu wa taarifa zinazoripotiwa nchini Uganda. Kiungo huyo mwenye uzoefu mkubwa kwa sasa anakipiga katika kikosi cha Singida Black Stars, huku klabu hizo mbili za Kenya zikifuatilia kwa karibu uwezekano wa kumpata katika dirisha hili la usajili

Simba yaibomoa Stellenbosch

Picha
Klabu ya Simba SC wapo kwenye mazungumzo ya kumchukua Ibraheem Jabaar Na Tayari wameweka Ofa Nono Mezani kwa ajili ya Midfielder hii hatari kutoka Stellenbosch FC Ya Afrika Kusini Ibraheem anaweza kucheza maeneo matatu ya mbele, number 8, number 10 na winga zote mbili kushoto au kulia. Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba Ibraheem Jabaar ni pendekezo la kocha Steve Baker ambae Alimsajili akiwa kama kocha wa Stellenbosch FC...

Simba hawalazi damu

Picha
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa kikosi chao hakina muda wa kupoteza ambapo mara baada ya ushindi mnono dhidi ya Mtibwa Sugar, timu hiyo ilisafiri usiku huohuo kutoka Morogoro kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya kuingia kambini moja kwa moja. Simba sasa inaelekeza nguvu zote kwenye mchezo wa raundi ya 29 wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Black Stars, mtanange utakaopigwa Jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kuanzia saa 10:00 jioni. ​Ahmed amefunguka kuwa kwa sasa klabu hiyo imeweka pembeni mpango wa kucheza soka la kuvutia au kuonyesha mbwembwe uwanjani, bali nguvu zote zimeelekezwa kwenye kusaka alama tatu muhimu pekee Aliongeza kuwa mbinu hiyo ya kucheza soka la moja kwa moja (direct football) ilianza kutumika tangu raundi ya 25 kutokana na mazingira magumu ya viwanja vya mikoani kama Jamhuri, pamoja na ukweli kwamba wanakutana na timu zinazopambana kufa na kupona kujinasua kutoka janga la kushuka daraja. ​Kuelekea mc...

Yanga yaikandika Azam FC 3-0

Picha
MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara nuliofanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jioni ya leo. Mabao ya Yanga yamefunwa na beki Ibrahim Hamad Abdullah ‘Bacca’ dakika ya 41, mshambuliaji Laurindo Dilson Maria AurĂ©lio ‘Depu’ kutoka Angola dakika ya 73 na kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua dakika ya 81. Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 69 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili ya watani wao, Simba baada ya timu hizo zote kucheza mechi 28 kuelekea mechi mbili za kukamilisha Kwa upande wao Azam FC baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 58 wakibaki pia katika nafasi ya tatu mbele ya Singida Black Stars yenye pointi 50 kufuatia timu hizo nazo kucheza mechi 28.

Simba yailowesha Mtibwa Sugar

Picha
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Mabao ya Simba SC yamefungwa na beki Rushine De Reuck kutoka Afrika Kusini kwa penalti dakika ya tisa, mshambuliaji mzawa, Suleiman Abdallah Mwalimu dakika ya 77 na winga Muivory Coast, Alain Anicet Oura dakika ya 90 Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 67, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga SC – wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 27 na kushukia nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16 kufuatia timu zote kucheza mechi 28. Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu. Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani n...

Yanga wanamrudisha tena Aziz Ki

Picha
Klabu ya Young Africans SC imetuma ofa rasmi ya USD 350K (Tshs Milioni 920) kwenda Al Ittihad SC ya Libya ili kupata saini na huduma ya kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki (30). KI Aziz amekubali kuitumikia Young Africans SC kwa mara nyingine tena baada ya kuondoka klabuni hapo na kujiunga na Wydad AC na baadae kusajiliwa na Al Ittihad SC ya Libya na klabu ya Young Africans inapambania hili ili kupata saini yake kwa wakati.