Libasse Gueye anauzwa
Klabu ya Simba SC inadaiwa kupokea ofa mbili kutoka nje ya Tanzania kwa ajili ya winga wake wa Senegal, Libasse Gueye.OFA ya kwanza imetoka kwa klabu ya Morocco yenye thamani ya $500,000 (takribani Sh bilioni 1.3), wakati ofa ya pili kutoka klabu ya Qatar inatajwa kuwa na thamani ya $700,000 (takribani Sh bilioni 1.8).
Hata hivyo, Simba inadaiwa kuwa tayari kumuuza nyota huyo endapo italetewa ofa ya $1,000,000 (takribani Sh bilioni 2.6).Endapo Libasse Gueye ataondoka Msimbazi, Simba inatarajiwa kuelekeza nguvu zake kwenye usajili wa winga mwingine wa kigeni ili kuziba nafasi yake katika kikosi.
