Tuliwazuia Simba- Nahodha Jamus
Nahodha wa Jamus SC ya Sudan Kusini, Kevin Muhire, amesema walifanikiwa kuizuia Simba kwa kuwabana nyota wake Clatous Chama na Inno Loemba katika mchezo wa Kombe la CECAFA Kagame uliochezwa Kigali, Rwanda.
Muhire amesema walitambua ubora wa Simba na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi yaliyolenga kuwazuia viungo hao kutengeneza mashambulizi.
"Tulijua Simba ni timu nzuri na ilihitaji pointi tatu, lakini tulifuata mpango wetu na tukapata pointi moja,".
Baada ya michezo miwili ya Kundi B, Jamus SC inaongoza kwa pointi nne, Singida Black Stars ina tatu, Simba mbili na Mogadishu City moja.
Matumaini ya Simba kutinga nusu fainali sasa yanategemea kuifunga Singida Black Stars katika mchezo wa mwisho wa makundi.
Hata hivyo, ushindi pekee unaweza usitoshe, kwani italazimika pia kusubiri matokeo ya mechi kati ya Jamus SC na Mogadishu City ili kujua hatma yake kwenye mashindano
