SAJILI ZA MAJINA MAKUBWA...

Na Prince Hoza Matua

PETER Shalulile ni jina kubwa lililotambulishwa mwanzoni mwa wiki hii ikiwa ni usajili wa klabu ya Yanga SC, huo ni usajili wa nne kati ya maproo waliowasajili msimu huu na kwa mujibu wa viongozi bado wachezaji wakubwa kuwatsngaza.

Shalulile ni mchezaji mkubwa barani Afrika, alikuwa anaichezea timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji walioipa jina timu hiyo kutokana na mafanikio yake.

Rekodi nzuri ya kufunga hasa kwenye ligi za ndani na kimataifa imemuweka kwenye wakati mzuri kama mchezaji, Shalulile ni mshambuliaji wa kati alikuwa na wastani wa kufunga magoli zaidi ya 20 hivyo aliibuka kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Shalulile amewahi kubeba CAF Champions League, pia ameshinda mara kadhaa ubingwa wa nchi hiyo na makombe mengine  ya ndani, ni mmoja kati ya wachezaji wenye sifa kemkem nchini humo.

Sidhani kama kuna timu nje ya Afrika Kusini ambayo haina shauku na mchezaji huyo mwenye uraia wa Namibia, Yanga SC ya Tanzania imekuwa ni timu nyingine iliyopata kummiliki mchezaji huyo badala ya Mamelodi.

Kwa mujibu wa Injinia Hersi ambaye ni Rais wa klabu hiyo, alikaririwa akisema ametumia miaka kadhaa kuwasiliana na mchezaji tena akitamani ajiunge na Yanga bila mafanikio.

Injinia Hersi amesema Shalulile alimpa matumaini ya kuja Yanga mkataba wake ukimalizika, jambo ambalo limetimia, usajili wa Shalulile unataka kuibua sajili za majina makubwa kwenye ligi yetu ama Yanga na Simba.

Baada ya Yanga kumleta Shalulile, watani zao Simba na wao wamesikika kutaka kuleta mchezaji mwenye jina kubwa anayecheza barani Afrika, Simba kupitia Kwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Crescentius  Magori amesema wanamsajili mchezaji mkubwa barani Afrika.

Kauli hiyo ya Magori inanihakikishia kwamba usajili wa sasa ni majina makubwa, bila shaka Yanga na wao watafanya muendelezo wa kusajili mchezaji mwenye jina kubwa bila kuangalia ubora wake wa sasa ndani ya peach.

Nikianza na Shalulile ni usajili wa kufuata jina kubwa na sio parfomance yake msimu uliopita, mchezaji huyo hakuwa na rekodi nzuri msimu uliopita hasa baada ya kufanikiwa kufunga magoli matatu.

Kuna tetesi nao Simba wanamleta Fiston Mayele raia wa DR Congo, ambaye amewahi kuichezea Yanga ya Tanzania, Mayele pia alikuwa anaichezea Pyramids ya Misri ambaye ameiwezesha timu hiyo kushinda taji la Afrika na la Misri.

Ingawa tetesi hizo zimezagaa sana jijini Dar es Salaam, lakini mchezaji mwenyewe amesababisha uvumi huo baada ya kuaga Pyramids, kwingine anakodaiwa kwenda ni Libya.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI