Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2026

Alphonce Mabula atambulishwa JS kabyile

Picha
Kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Alphonce Mabula Msanga ametambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa klabu ya JS Kabylie ya Nchini Algeria kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na klabu ya Şamaxı FK ya Azerbaijan kusikia ukomo. Klabu hiyo imethibitisha kukamilisha usajili wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 leo Agosti 31, 2026 kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii bila kuweka wazi urefu wa mkataba wake klabuni hapo.

Simba yaikaba koo Yanga kileleni

Picha
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC ya mitaa ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam usiku huu imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold FC katika uwanja wa Meja Isamuhyo Mbweni jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo wa mfululizo wa Ligi Kuu bara ikiwa ni raundi ya tano, mabao ya Simba yalifungwa na viungo Clatous Chama na Libasse Gueye ambaye alitoa assist wakati Chama anafunga na kuandikisha assist yake ya tano kwenye ligi hiyo. Kwa ushindi wa leo Simba imefikisha alama 15 ikiwa imefunga mabao 9 inashika nafasi ya pili nyuma ya Yanga.

Mabedi kuwaongoza mabaya wa Simba

Picha
Kocha msaidizi wa zamani wa Yanga, Patrick Mabedi, ataiongoza Mighty Wanderers ya Malawi kwenye mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Simba ya Tanzania, mwishoni mwa juma hili, akichukua nafasi ya kocha Bob Mpinganjira aliyesimamishwa kazi. Kocha Mpinganjira amesimamishwa kazi na mabingwa hao wa Malawi baada ya jana kupoteza mchezo wa fainali ya michuano ya Airtel Top 8 kwa kufungwa mabao 2-1 na timu ya Ekhaya FC. Maamuzi ya kumpa kazi hiyo Patrick Mabedi yamekuja muda mchache baada ya timu hiyo kumsimamisha kazi kocha Bob Mpinganjira, na mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya Simba katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika mwishoni mwa juma hili. Taarifa zinadai kocha Patrick Mabedi amepewa jukumu la kuhakikisha Mighty Wanderers inaitoa Simba na kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika. Akiwa kocha msaidizi wa Yanga ndani ya msimu mmoja, kocha Mabedi alicheza michezo mitatu dhidi ya Simba ambapo alipoteza mchezo mmoja ...

Yanga yazidi kupaa kileleni

Picha
Young Africans maarufu Yanga SC yenye maskani yake mitaa ya Jangwani jijini Dar es Salaam, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. Mchezo huo wa Ligi Kuu bara, Yanga iliandika mabao hayo kupitia kwa Peter Shalulile na Mudathir Yahya, kwa matokeo hayo Yanga insfikisha pointi 15 ikiwa imecheza mechi 5 na imefunga mabao 15.

Tanzania kuandaa AFCON U20 Septemba

Picha
Kura za michuano ya kufuzu AFCON kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 kanda ya CECAFA zimepigwa rasmi mjini Kigali, huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa itakayopigwa mwezi Septemba. Tanzania imepangwa pamoja na Ethiopia na Rwanda, ikiwa ni kundi lenye ushindani mkubwa wa Afrika Mashariki. Kundi B linawakutanisha Uganda, Sudan, na Djibouti, wakati Kundi C linajumuisha South Sudan, Kenya, na Burundi. Vinara wa makundi yote matatu pamoja na mshindi wa pili aliye na matokeo mazuri zaidi watatinga hatua ya nusu fainali. Timu mbili za mwisho zitakazochuana kwenye fainali ndizo zitakazowakilisha kanda ya CECAFA katika michuano ya AFCON U-20 2026.

CAF yazitaka klabu shiriki mashindano yake kuandaa bajeti

Picha
CAF imeziomba klabu 115 zinazoshiriki CAFCL na CAFCC kuandaa bajeti stahiki za kina za gharama za usafiri kwa msimu mpya wa 2026-27 na kuziwasilisha kwa shirikisho hilo. Mkutano huo ulifanyika Jumapili hii iliyopita na kuongozwa na Mwenyekiti wa ACA na Rais wa Young Africans SC Eng Hersi Said ili kupunguza gharama za vifaa na fedha. Eng Hersi Said alihakikisha kuwa Rais wa CAF Patrice Motsepe amejitolea kutafuta suluhisho la changamoto hizo na lengo kuu ni kurahisisha usafiri, kupunguza gharama zisizo za lazima na kuboresha hali za klabu katika mashindano hayo ya kimataifa. Mkutano huo uliandaliwa na ACA kwa lengo la kutafuta suluhisho la Ugumu wa Usafiri katika mashindano ya Bara.

Djuma Shabani: Beki wa kulia aliyepita Young Africans

Picha
‎Djuma Shabani, alizaliwa Machi 16, 1993 huko Kindu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ni mwanasoka wa kulipwa kutoka DR Congo anayecheza nafasi ya beki wa kulia. ‎Djuma ni moja ya Wachezaji wakubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukaba, kupandisha mashambulizi, na kupiga penalti. ‎ ‎Djuma alianza soka lake la ushindani katika klabu mbalimbali nchini mwake DRC kabla ya kusajiliwa na FC Renaissance du Congo ambapo alikuwa nahodha na nguzo muhimu ya ukuta. Baadaye alihamia klabu kubwa ya AS Vita Club mwaka 2017. ‎ ‎Akiwa na AS Vita Club Djuma alipata mafanikio makubwa yakiwemo Kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya DRC (Linafoot) msimu wa 2017–18, Kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAF Confederation Cup) mwaka 2018 kabla ya kupoteza mbele ya Raja Casablanca ya Morocco. ‎ ‎Juni 2021, Djuma Shabani alihamia rasmi nchini Tanzania na kusaini mkataba na klabu ya Young Africans . Katika kipindi chake akiwa Yanga, alijinyakulia upendo mkubwa kutoka kwa mash...

Depu aanza na goli Petro de Luanda

Picha
Mshambuliaji wa zamani wa Young Africans, Laurindo Depu, leo ameanza kuonyesha makali yake baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa 2-0 wa Petro de Luanda dhidi ya Académica do Lobito kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Angola. Hili ni bao lake la kwanza Depu tangu ajiunge na miamba hiyo ya Angola.

Maua Sama kuwa mama mtarajiwa

Picha
Msanii wa Bongo Flava Maua Sama ameamua kuwafahamisha mashabiki zake kuwa anatarajiwa kuwa mama hivi karibuni baada ya ku-share picha zake mpya ambazo zimemuonyesha akiwa mjamzito baada ya tetesi kusambaa mitandaoni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Maua ameweka picha hizo akisindikiza na ujumbe uliosomeka, “Am grateful Alhamdulillah, post ambazo imepata comments mbalimbali za wasanii na mashabiki zake wakimpa hongera na kumtakia kheri. Maua Sama

Nabi ajiuzuru

Picha
Kocha Nasreddine Mohammed Nabi, rasmi amejiuzulu nafasi yake ya kocha mkuu ndani ya Raja CA baada ya kinachosemwa kutofautiana na mkurugenzi wa michezo "sporting director" wa klabu hiyo. Moja ya makubaliano ambayo Nabi alitilia mkazo wakati anasaini mkataba ni pamoja na kuhusishwa kwenye usajil wa wachezaji wapya ikiwemo matakwa yake yeye na moja ya wachezaji aliowakosa na kupelekea mzozo ni Thapelo Maseko ambaye ametimkia Copenhagen Nabi alikua anamtaka huku Sporting Director anasema hafai kwenye mpango wa klabu Nabi amehudumu ndani ya Raja CA kwa muda wa miezi 2 na nusu sawa na siku 78 tu tangu alipoteuliwa June 12, 2026 Kwasasa Nabi yuko zake huko Brussels, Ubelgiji kupumzika lakini kusikilizia majibu ya uongozi wa Raja CA kuhusu barua yake

Steve Barker aihofia safu ya ushambuliaji Geita

Picha
Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi kuwa kikosi chake kinakabiliwa na changamoto ya kuwakosa wachezaji kadhaa katika mchezo unaofuata dhidi ya Geita Gold, huku akiahidi kuwa wamejipanga vizuri kwa ajili ya ushindani huo. Barker ameeleza kuwa kuna idadi kubwa ya wachezaji wanaoweza kukosa mchezo huo kuliko inavyofikiriwa, kutokana na adhabu na majeraha mbalimbali. Amesisitiza kuwa kukosekana kwa wachezaji hao ni sehemu ya mchezo na benchi la ufundi linaendelea kujiandaa vyema ili kuwa tayari kukabiliana na Geita Gold. Akizungumzia wapinzani wao, kocha huyo amekiri kuwa Geita Gold ni timu nzuri, iliyofundishwa vyema na inayojua kufunga mabao, hivyo anatarajia mchezo mgumu wenye ushindani wa hali ya juu.

Dube atakata Hardrock

Picha
Prince Dube na Hardrock FC wametinga hatua ya robo fainali baada ya kuwatwanga kama mihogo Jordan Sinoti kwenye kombe la Munhumatapa Challenge Cup Katika mchezo huo Dube aliianza lalini hakufamikiwa kufunga kwenye karamu ya mabao 5-1 FT: Hardrock 5-1 Jordan Sinoti

Kocha Geita Gold aizimia Simba

Picha
Kocha wa Geita Gold, Zubery Katwila, amesema kesho wanakutana na timu bora ambayo inaendelea kuimarika zaidi kiuchezaji dimbani. Katwila amesema kadri siku zinavyosonga, Simba inaendelea kuwa bora zaidi, hivyo wao kama Geita Gold wamejiandaa na mbinu zitakazowasaidia kufanya vizuri. Pia amesema watajaribu kutumia makosa ambayo Simba itafanya ili kuwapa adhabu uwanjani na kutafuta matokeo mazuri.

Magori atamba kuifunga Geita Gold kesho

Picha
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba SC, Crescentius Magori akielezea mchezo dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kupigwa tarehe 31.8.2026 pale Meja Gen. Isamuhyo. "Kila mchezo tunaocheza tukiwa nyumbani hakuna budi kushinda, kwa maana mechi zote tushinde tukiwa nyumbani kama tulivyoshinda za ugenini. "Pia timu kama Geita FC, kwetu sisi ni kama marafiki, kwa hiyo utakuwa mchezo ambao tunapambana na timu tunayoijua vizuri". Anaongeza kuwa "Nasema hivyo kulingana na timu yetu tuliyo nayo. kucheza mechi moja na kupoteza sio ndio kushindwa, ila ndio mwanzo mzuri wa kujua wapi tumekosea, wapi tuboreshe. *Tazama mchezo wetu dhidi ya Coastal Union, tulicheza vizuri bila kadi yoyote nyekundu kama mechi za ugenini. "Tunahitaji kuweka heshima, ndio kila kitu kwenye mpira, kwa hiyo na hilo tumelishughulikia vikali na sasa tunashinda kama kawaida", Anamaliza.

Mbwana Samatta afunga bao la msimu

Picha
Nahodha wa zamani wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amefungua akaunti yake ya magoli kwenye Ligi Ligi kuu Ufaransa (Ligue 1) na kuisaidia timu yake ya Le Havre kuondoka na alama moja kwenye sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Olympique Lyon. Le Hevre walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa Nahodha wa zamani wa Tanzania, Mbwana Samatta dakika ya 74 kabla ya Lois Openda kuisawazishia Lyon dakika ya 87 na kufanya timu hizo kugawana alama moja

Ronaldinho Gaucho arejea kwenye soka na mabao

Picha
Miaka 11 baada ya kuaga soka la ushindani, Ronaldinho Gaúcho amerudi tena kwenye soka la kulipwa akiwa na miaka 46 Nguli huyo wa Brazil amejiunga na Ravenna FC ya Italia, inayoshiriki Serie C, akiwa tayari kutoa mchango wake kwa timu hiyo. Cha kuvutia zaidi, Ronaldinho ameacha mlango wazi wa kucheza angalau mchezo mmoja rasmi, huku akitamani kufikisha bao lake la 300 katika soka la kulipwa. Mechi ya kwanza katokea Sub katupia chuma mbili kumbe miaka inaweza kupita, lakini uchawi wa Gaucho hauzeeki.

Allasane Kante atemwa Simba

Picha
Jioni ya leo Klabu ya Simba imemuaga kiungo wake Allasane Kante, katika mchakato wa maboresho na mabadiliko ndani ya kikosi cha Mnyama. Lakini binafsi, niliona bado Kante alikuwa na nafasi pale Msimbazi. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kukaba, kushinda mipira na kuanzisha mashambulizi, hasa kupitia pasi zake zenye ubora. Wakati mwingine kwenye maboresho ya kikosi, si kila anayeondoka alikuwa hafai. Kante alikuwa na kitu chake ndani ya uwanja. Huenda Simba wameona kitu kingine mbele, lakini kwangu mimi, kumuacha Kante ni uamuzi ambao bado utahitaji kuthibitishwa na matokeo.

Oruma aiponda Yanga, aifagilia Simba

Picha
Mchambuzi wa michezo Wilson Oruma ametoa kauli nzito kuhusu ubora wa kikosi cha Yanga SC, akidai kuwa timu hiyo haina kikosi cha kutosha kwa ushindani wa msimu huu. Oruma ameenda mbali zaidi kwa kutoa utabiri kwamba Simba SC itatwaa ubingwa, akiamini itakuwa na tofauti ya pointi 10 mbele ya Yanga. Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki wa soka, huku msimu ukiwa bado katika hatua za mwanzo na timu zikiendelea kupambania alama.  Wilson Oruma

Singida BS yaishushia lundo la magoli Polisi Tanzania

Picha
Timu ya Singida BS usiku huu imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Polisi Tanzania katika uwanja wa Airtel uliopo mjini Singida mchezo wa Ligi Kuu bara. Ilianza Polisi kupitia Baraka Michael na goli lao la pili lilifungwa na Ibrahim Ame. Wenyeji Singida BS wakafungua karamu ya magoli kupitia Jonathan Sowah, kisha James Mwashinga, Shekhan Ibrahim na baadae Jeancy Mboma akaweka goli la nne.

Said Mtanda aisifu Pamba Jiji kufungwa 2-0 na Yanga

Picha
Licha ya Pamba Jiji FC kupokea kwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa jana, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mlezi wa klabu hiyo, Said Mtanda— ambaye pia ni shabiki wa damu wa klabu ya Yanga SC ameeleza kuridhishwa kwake na kiwango kilichoonyeshwa na timu hiyo. Mtanda ameeleza kuwa watu wengi walidhani Pamba Jiji ni timu dhaifu na ingekubali kipigo kizito cha magoli matano (5) au zaidi kutoka kwa Yanga SC, lakini wameonyesha ushindani mkubwa uwanjani. Kilichomfurahisha zaidi ni uamuzi wa kocha kuwatumia wachezaji sita (6) kutoka kikosi cha vijana cha U-20 kwenye mchezo huo dhidi ya Mabingwa watetezi Yanga. Mtanda ametoa kauli hizo baada ya kushuhudia mchezo wake wa mwisho kabla ya kuondoka Mwanza, na kuelekea Mkoa wa Simiyu kuendelea na majukumu yake.

Geita Gold yaifuata Simba na ndege

Picha
Kikosi cha Geita Gold FC kimewasili rasmi jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa ndege ya Air Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya michezo yao miwili mikubwa ya NBC Premier League dhidi ya miamba ya soka nchini, Simba SC na Yanga SC. Hii ni mara ya pili msimu huu kwa Geita Gold kutumia usafiri wa anga kusafiri kuelekea mechi zao ili kuwapa wachezaji mapumziko ya kutosha na kuepuka athari za safari ndefu za barabarani.

Maxi Nzengeli afichua siri za Simba

Picha
Kiungo mshambuliaji raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Maxi Mpia Nzengeli, amefichua kuwa Simba SC ndiyo iliyokuwa klabu ya kwanza kabisa kutoka Tanzania kuonyesha nia ya dhati na kutuma ofa rasmi ya kumhitaji kutoka AS Maniema Union. Akizungumza kupitia podcast ya The Physics inayozungumzwa na Denis Nkane, Maxi alieleza kuwa ingawa Simba ilitangulia, mazungumzo na taratibu zao hazikufikia mwafaka au kwenda kama ilivyotarajiwa, hali iliyotoa fursa kwa Yanga SC kuingia kwenye mbio hizo na kufanikisha saini yake. ​Akifafanua zaidi kwenye mahojiano hayo, Maxi alibainisha kuwa njia yake ya kuelekea Yanga SC ilirahisishwa zaidi na mahusiano mazuri na ya karibu ya kibiashara yaliyokuwepo kati ya bosi wa AS Maniema Union, Jenerali Amisi Kumba, na uongozi wa Yanga. Ushirikiano huo ulikuwa umeimarika kufuatia mafanikio ya usajili wa wachezaji waliotangulia kufanya vizuri kutoka DRC kama Fiston Mayele na Tuisila Kisinda. Kwa kuwa uongozi wa Maniema Union ulimchukulia Maxi kama mtoto wa fa...

Manqoba asikitikia kukosa mabao

Picha
Kocha mkuu wa Yanga SC Manqoba Mngqoithi raia wa Afrika Kusini, anasikitishwa na timu yake kushindwa kutumia nafasi na kuondoka na ushindi mkubwa wa mabao. Kocha huyo ameonesha kusikitishwa kwake na wachezaji wake ingawa anaamini ipo siku wachezaji wake watabafilika na kuibuka na ushindi mkubwa. Mpaka sasa Yanga imefunga jumla ya mabao 13 ikiwa ndio kinara kwa kufunga mabao mengi ikifuatiwa na Geita Gold yenye mabao 9 na Simba yenye mabao 5. "Nipo hapa Kwa Wiki Sita tu, Sijafurahishwa na Idadi ya Magoli, Tumefunga Magoli 13 Tu kwenye mechi 4 hiyo sio sawa Kwa Level Yangu, ninafuraha tu Kwasababu najua ipo Siku Kuna Mtu Tutamfunga Goli Nyingi na Itakuwa sio sawa kwake lakini ndio Mpira" Ameyasema Hayo Kocha Mkuu wa Yanga Manqoba Mngoith.

Yanga mwendo mdundo ikiilalua Pamba Jiji

Picha
Timu ya Yanga SC usiku huu imeendelea kuchanja mbuga kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo Yanga inaendeles kukaa kileleni ikifikisha pointi 12 huku ikiwa imefunga mabao 13 huku ikicheza mechi 4. Yanga ilianza kupata bao kupitia kwa Maxi Nzengeli assist ya Sheikh Ibrahim Toure dakika ya 17 kabla ya Toure kufunga la pili assist ya Peter Shalulile dakika ya 23. Yanga sasa itasafiri tarehe 1, Septemba kuwafuata Fountain Gate wanaotumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Wachezaji 15 Afrika wanaolipwa zaidi, Girumugisha ashika ya 3

Picha
Jean Claude Girumugisha amekuwa mchezaji wa tatu anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika historia ya soka barani Afrika, ikiwa tunazingatia mishahara inayolipwa katika mashindano ya ndani ya Afrika pekee. Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Story Africa, hawa ndio wachezaji wanaodaiwa kulipwa mishahara mikubwa zaidi katika historia ya soka la ndani barani Afrika: 1. Fiston Mayele — analipwa dola milioni 5 kwa mwaka na Al Ahli Tripoli. 2. Mohamed Tougai — analipwa dola milioni 3.7 kwa mwaka na Al Ahli Tripoli. 3. Jean Claude Girumugisha — analipwa dola milioni 2.4 kwa mwaka na Al Ahli Tripoli . 4. Ferjani Sassi — aliwahi kulipwa dola milioni 2.2 kwa mwaka na Zamalek kati ya 2018 na 2021. 5. Ali Maaloul — aliwahi kulipwa dola milioni 1.5 kwa mwaka na Al Ahly kati ya 2021 na 2025. 6. Anthony Modeste — aliwahi kulipwa dola milioni 1.5 kwa mwaka na Al Ahly kati ya 2023 na 2024. 7. Ramadan Sobhi — analipwa dola milioni 1.446 kwa mwaka na Pyramids FC tangu 2020. 8. Youcef Belaïli — aliwahi k...

Enzo aondolewa Chelsea

Picha
Kiungo wa Chelsea, Enzo Fernández, ameondolewa rasmi kwenye kikosi cha Chelsea usiku wa leo Agosti 27, katika mchezo wa Carabao Cup dhidi ya Luton Town, baada ya kukubali maslahi binafsi na kutoa "Green Light" kuhamia Manchester City. Enzo Fernández amevutiwa sana na mradi wa Manchester City na amewaambia mawakala wake kuwa anataka kuhamia Etihad. Kocha mpya wa Man City, Enzo Maresca, amemtaja Enzo kama shabaha yake namba moja ili kuziba pengo la Rodri aliyetimkia Barcelona. Wawili hao walifanya kazi kwa mafanikio makubwa hapo awali ndani ya Chelsea.

Mwamuzi wa kwanza mwanamke Afrika Kusini atajwa FIFA

Picha
Akhona Zennith Makalima (aliyezaliwa tarehe 27 Machi 1988, mwenye umri wa miaka 37) ni mwamuzi wa kimataifa wa soka kutoka Afrika Kusini, ambaye amekuwa kwenye orodha ya waamuzi wa kimataifa wa FIFA tangu mwaka 2014. Anachezesha mechi chini ya FIFA, CAF, COSAFA, Premier Soccer League (PSL), pamoja na Shirikisho la Soka la Afrika Kusini (SAFA). Alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa mwamuzi katika Premier Soccer League. Ana Diploma ya Kitaifa ya Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka King Hintsa FET College, na kwa sasa anafanya kazi kama msimamizi katika Idara ya Michezo. Tarehe 9 Januari 2023, FIFA ilimteua kuwa sehemu ya kundi la waamuzi kwa Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA 2023 lililofanyika Australia. Pia alikuwa mwamuzi wa VAR katika AFCON 2023, na alifanya kazi kama mwamuzi wa VAR katika CAF Super Cup 2024.

Sele Gomez aja na muonekano mpya

Picha
Straika mpya wa Yanga SC, Selemani Mwalimu ‘Gomez’, akiwa mazoezini na mwonekano mpya. Kwa mujibu wa taarifa ya Yanga, kesho mshambuliaji huyu atakuwa uwanjani wakati Yanga wakikipiga dhidi ya Pamba Jiji FC. “Chuma kipo tayari kwa ajili ya kuwapa furaha Wananchi Kesho,” taarifa ya Yanga SC.

Simba yapata ushindi kiduchu

Picha
Timu ya Simba SC usiku huu imepata ushindi kiduchu baada ya kuifunga Coastal Union ya Tanga bao 1-0 katika uwanja wa Meja Isamuhyo Mbweni jijini Dar es Salaam. Mchezo huo wa Ligi Kuu bara ulikuwa wa upande mmoja kwa Simba kufanya mara kwa mara, bao pekee la Simba limefungwa na Ismail Toure baada ya kutokea nyuma.

Bodi ya Ligi Tanzania na Mali waenda kujifunza Yanga

Picha
Uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ukiambatana na wageni wao kutoka Bodi ya Ligi ya Mali, umefika katika Klabu ya Yanga kwa ziara yenye lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu namna klabu inavyojiendesha. Katika ziara hiyo, wageni hao wamepata fursa ya kufahamu mifumo ya uendeshaji wa klabu, usimamizi wa shughuli za kila siku, maendeleo ya biashara na masoko, matumizi ya teknolojia, pamoja na namna Yanga inavyosimamia chapa yake na kuwahudumia mashabiki Wageni hao wamepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Yanga SC, Andre Mtine