Yanga yazima tetesi za Feitoto kutua Yanga'

Baada ya kuzagaa kwa tetesi zinazomhusisha kiungo wa Azam FC, Feisal Salum, na kujiunga na Yanga, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Kamwe, amesema hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea kati ya pande hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kamwe amesema Yanga tayari imekamilisha usajili wa wachezaji wa ndani, hivyo Feisal si sehemu ya mipango ya klabu hiyo.

"Feisal Salum ni mchezaji mzuri sana, lakini Yanga SC tumeshafunga usajili wetu wa ndani. Hakuna mazungumzo yoyote kati ya Yanga na Fei/Azam," ameandika Kamwe.

Aidha, ameeleza kuwa nafasi mbili za usajili zilizobaki klabuni hapo ni kwa ajili ya wachezaji wa kimataifa pekee.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons