Girumugisha aikwepa Yanga na kutimkia Libya
Winga Jean Claude Girumugisha amewasili nchini Libya kwaajili ya kukamilisha mchakato wake wa usajili wa kujiunga na Al Ahli Tripoli akitokeaAl Hilal Omdurman kwa msimu mpya!
Jean Claude Girumugisha hatajiunga na Young Africans SC kuelekea msimu ujao wa 2026-27 ambao waliulizia thamani ya winga huyo na hawakurudi tena mezani kupambania saini na huduma ya mchezaji huyo ambaye amekuwa na misimu bora sana
