Mayele aaga Pyramids, ahusishwa Simba

Mshambuliaji Fiston Mayele ameaga rasmi Pyramids FC baada ya kumaliza safari yake ya miaka mitatu ndani ya klabu hiyo.

Mayele ameondoka akiwa mchezaji huru, huku akitoa shukrani kwa viongozi, wafanyakazi, wachezaji wenzake na mashabiki wa Pyramids FC kwa imani na sapoti waliompa wakati wote aliokuwa klabuni hapo.Mayele: "

Kila stori ina mwisho wake lakini kumbukumbu zinadumu milele. Asante kwa Rais, wafanyakazi, wachezaji wenzangu, mashabiki na kila mmoja aliyekuwa na imani na mimi tangu ujio wangu."

Katika kipindi chake Pyramids FC, Mayele amefanikiwa kutwaa mataji manne, akiwemo taji moja la ndani na mataji matatu ya kimataifa.

Sasa akiwa mchezaji huru, swali kubwa kwa mashabiki wa soka Tanzania ni kama Simba SC inaweza kuwa moja ya klabu zitakazopigania saini yake

Tetesi za usajili wa Mayele zimeanza kuhusishwa na mipango ya Simba ya kufanya usajili mkubwa kuelekea msimu mpya, hasa baada ya Yanga SC kuendelea kuimarisha kikosi chake kwa usajili wa nyota mbalimbali.Hata hivyo, hadi sasa hakuna uthibitisho rasmi kwamba Simba SC imefikia makubaliano.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI