Mbegu wa Simba kupaa Czech
Muda wowote kuanzia sasa kinda wa Simba,Hussein Ally Mbegu (17) atapaa kwenda Czechia ili kufanya majaribio ya wiki mbili na klabu ya Slavia Prague.
Simba wametoa ruhusa ya Mchezaji huyo kwenda Czechia ili kujaribu baati yake na kama atafuzu biashara itafanyika.
Kwa sasa Mchezaji huyo anahangaikia Viza na muda siyo mrefu ataondoka nchini. Kama biashara hiyo itafanikiwa Simba wataweka kipengele cha “sell-on clause” kama walivyofanya kwa Mbwana Samatta siku za karibuni.
