Ben Lee atua Tanzania


Tanzania imepiga hatua nyingine katika juhudi za kuendeleza mchezo wa uogeleaji kufuatia kuwasili kwa kocha wa kimataifa, Ben Lee, ambaye atatoa mafunzo ya kiwango cha kimataifa kwa waogeleaji, makocha na wazazi.

Mafunzo hayo yatafanyika kupitia programu maalumu iliyoandaliwa na Monti International School.

Ujio wa Ben Lee unaelezwa kuwa ni hatua muhimu katika safari ya kuinua viwango vya uogeleaji nchini kwa kuwaletea Watanzania utaalamu wa kimataifa bila kulazimika kusafiri nje ya nchi.

Kocha huyo ana uzoefu mkubwa wa kuwafundisha waogeleaji walioshiriki mashindano ya NCAA na Olimpiki.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mapokezi ya kocha huyo jijini Dar es Salaam, Afisa Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Petro Gallos mbali na kupongeza ujio wake, amesema wakufunzi wa ndani wa mchezo huo wanapaswa kutumia mwanya huo adhimu kwa kuchota ujuzi wenye manufaa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons