Bodi ya Ligi kuanzisha sheria mpya kwa wachezaji wa kigeni
Bodi ya Ligi Tanzania inatarajiwa kuanzisha kanuni mpya ya usajili wa wachezaji wa kigeni itakayoanza kutumika kuanzia msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya NBC.
Kwa mujibu wa kanuni hiyo mpya, mchezaji wa kigeni atakayehitaji kusajiliwa na klabu yoyote ya Ligi Kuu ya NBC atalazimika kuwa ameiwakilisha nchi yake katika timu ya taifa ya U-17, U-20 au timu ya taifa ya wakubwa, kuanzia mwaka 2024 na kuendelea, ili aweze kustahili kusajiliwa.
Hata hivyo, sheria hiyo haitawahusu wachezaji wa kigeni ambao tayari walikuwa wakicheza Ligi Kuu ya NBC katika msimu wa 2025/26 au misimu iliyotangulia. Hivyo, wachezaji hao wataendelea kustahili kucheza bila kulazimika kutimiza sharti hilo jipya.
