Sakata la Seleman Mwalimu lafikia pabaya

Mshambuliaji wa Simba SC Seleman Mwalimu ameondoka kambini kwa timu hiyo mjini Kigali, Rwanda, na kurejea Dar es Salaam huku hatma yake ndani ya kikosi hicho ikiendelea kujadiliwa.

Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Simba unatarajia kuanza mazungumzo na klabu ya Wydad Athletic Club ya Morocco kwa lengo la kufikia makubaliano yatakayomwezesha mshambuliaji huyo kuendelea kuitumikia Simba kwa msimu mmoja zaidi kwa mkopo.

Hata hivyo, endapo pande hizo mbili hazitafikia mwafaka, mchezaji huyo atalazimika kurejea Wydad, ambayo bado inamiliki haki za kimkataba za mshambuliaji huyo.

Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya jitihada za Simba kuhakikisha inaendelea kuwa na kikosi imara kuelekea msimu mpya wa mashindano.



Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons