Peter Shalulile asajiliwa na Yanga
Klabu ya Young Africans imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Namibia, Peter Shalulile, aliyekuwa akiitumikia Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Shalulile anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Yanga kama sehemu ya maboresho makubwa ya kuelekea msimu mpya, huku akitajwa kuziba pengo lililoachwa na mshambuliaji Prince Dube, ambaye ameondoka ndani ya klabu hiyo.
