Ahoua kimeeleweka Jordan

Mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2024/25, Jean Ahoua ametangazwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Al-Faisaly SC ya Nchini Jordan akitokea klabu ya CR Belouizdad ya Algeria.

Nyota huyo wa zamani wa Simba SC, raia wa Ivory Coast, amejiunga na klabu hiyo kwa uhamisho huru baada ya kusitisha mkataba wake na CR Belouizdad kwa makubaliano ya pande zote mbili, akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia miamba hiyo ya Jordanian Pro League.

Ahoua 24 alijiunga na Simba SC mnamo Julai 2024 na kuitumikia klabu hiyo Kwa msimu mmoja na nusu ambapo aliisaidia miamba hiyo ya Dar es Salaam kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2025 huku akiwa kinara wa magoli kwenye Ligi kuu bara akifikisha jumla ya magoli 16 kwenye ligi hiyo msimu wa 2024/25.

Mnamo Januari 2026 Simba SC alimuuza nyota huyo wa zamani wa Stella Club d'Adjamé ya Nchini kwao Ivory Coast kwenda CR Belouizdad na kuhudumu kwa miamba hiyo ya Algeria kwa nusu msimu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI