Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2024

Clara Luvanga azidi kung' ara Saudi Arabia

Picha
Mchezaji wa Tanzania, Clara Luvanga usiku wa jana ameiwezesha timu yake ya Al Nassr FC ya Saudi Arabia kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Al Amal katika mchezo wa Ligi Kuu. Kwenye mchezo huo Clara amefunga goli moja, ikumbukwe Clara alikuwa anaichezea Yanga Princess ya Tanzania na timu ya taifa, Twiga Stars.

Cedric Kaze amfuata Nabi Kaizer Chief

Picha
Klabu ya Kaizer Chiefs imemtambulisha rasmi Cédric Kaze kama kocha msaidizi wa klabu hiyo akiungana na kocha Nasreddine Nabi ambae ni kocha mkuu wa klabu hiyo. Wawili hao walikuwa pamoja kwenye klabu ya Yanga na wakaiwezesha kushinda mataji mawili ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara. Kukutana tena Kaizer Chief kunaweza kuisaidia timu hiyo kurejea kwenye ubora wao kama ilivyokuwa kwa Yanga.

Yanga haina majeruhi yoyote

Picha
Meneja wa kikosi Cha Yanga SC Walter Harrison amesema hakuna majeruhi yoyote kwenye kikosi chao zaidi ya Farid Mussa ambaye ameanza mazoezi. Kwa mujibu wa maneno ya Harrison, zinaondoa taarifa za kuumia Ibrahim Baka, kwamba watu waliovumisha kwenye Instagram hazina ukweli wowote. "Wachezaji wote waliokua kwenye majukumu ya timu za Taifa wapo vizuri,hakuna taarifa mpya kuhusu majeraha zaidi ya Farid Mussa ambaye ameanza mazoezi mepesi,wengine wote wapo sawa"Walter Harrison Meneja wa kikosi cha Yanga.

Sipendi kuangalia soka: CR7

Picha
STAA wa soka duniani, Cristiano Ronaldo amesema anapokuwa mbele ya runinga hapendi kuangalia soka. Ronaldo anasema: “Kucheza soka ni mapenzi yangu, lakini napendelea kutazama michezo mingine kwenye TV. Kati ya kutazama mechi ya mpira wa miguu au ndondi au UFC, mimi huchagua ndondi au UFC." Ikumbukwe huyu sio mchezaji wa kwanza kuikataa soka ya kwenye TV awali Gerard Pique aliwahi kusema inachosha kuangalia soka kwa dakika 90, pia De Lima alisema bora aangalie tenis kuliko soka.

Minziro kumrithi Kopunovic Pamba Jiji

Picha
Kocha Fred Felix Minziro atachukua mikoba ya Goran Kopunovic ambae amefutwa kazi Pamba JIJI FC, Minziro ataenda Pamba JIJI FC akiwa na wasaidizi wake akiwemo Mathias Wandiba ambae ameshafanya nae kazi Geita Gold FC. Kwasasa Mathius Wandiba yupo na kikosi cha Pamba JIJI FC.

MECHI YA SIMBA NA YANGA JMOSI ITAKUWA HIVI!

Picha
NA PRINCE HOZA WATANI wa jadi Simba SC na Yanga SC Jumamosi ijayo watashuka dimbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, mchexo wa Logi Kuu bara. Huu ni mchezo wa pili tangu zilizokitana mwanzoni mwa msimu kuwania Ngao ya Jamii, katika mchezo huo Yanga SC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Maxi Nzengeli katika dakika ya 6 kipindi cha kwanza. Kwenye mchezo huo, Simba SC itakuwa mwenyeji huo hivyo ina matumaini makubwa ya kuondoka na ushindi, lakini rekodi za watani hao, walikutana msimu jana ambapo Yanga SC iliibuka mshindi katika mechi zote mbili. Mzunguko wa kwanza Yanga SC iliibuka na ushindi wa mabao 5-1, huku Simba ikiwa mwenyeji, na kwenye mchezo wa marudiano Yanga tena iliibuka mshindi kwa mabao 2-1. SIMBA NA MATUMAINI MAKUBWA YA KUSHINDA Simba SC inayonolewa na Fadlu David's raia wa Afrika Kusini, ina matumaini makubwa ya kupata ushindi kwenye mchezo huo, matumaini ya Wanasimha yanatoka kwa wachezaji wao iliyowasajili mwanzoni mwa msimu huu. Laki

Ibrahim Baka kuikosa Simba Jumamosi

Picha
Kuna uwezekano mkubwa beki wa kati wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC Ibrahim Hamad "Baka" ataukosa mchezo wa watani dhidi ya Simba SC utakaochezwa Jumamosi uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Akipost kwenye mtandao wake wa Instagram, Baka ameandika kwamba ameumia katika mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya DR Congo ambapo timu ya taifa ya Tanzania ilifungwa mabao 2-0. Kukosekana kwake kwenye mchezo huo kunaweza kuwa pengo kubwa kwa Yanga ambao watakuwa wageni wa Simba katika mchezo huo ambao wanataka kulipa kisasi cha kufungwa mechi tatu mfululizo Baka ameumia

Samatta awajaza matumaini Watanzania kufuzu AFCON

Picha
Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta baada ya mchezo dhidi ya DR Congo waliopoteza 2-0 uwanja wa Taifa ameonyesha kuwa bado ana matumaini na timu ya Taifa. " Ipo siku vijana watakuwa bora na kutupa furaha wa-Tanzania." - Mbwana Samatta. Nyota huyo licha ya kuumia kwenye mchezo huo lakini hakujali aliendelea kuipigania bendera ya nchi kwa moyo na jasho lake lote. Stars imesaliwa na michezo miwili kwenye kampeni ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Guinea na dhidi ya Ethiopia.

Spiderman kuwafuata Yanga

Picha
Golikipa wa Klabu ya Simba, Moussa Camara ameanza safari kutokea Abidjan, Ivory Coast kuja Tanzania ili kuwahi maandalizi ya Dabi ya Kariakoo. Moussa Pinpin Camara amedaka michezo yote miwili dhidi ya Ethiopia kwa dakika 90 wakati Guinea ikishinda michezo hiyo yote. . #sokamagicupdates

Harmonize arekodi 3 kwa mpigo

Picha
Msanii Harmonize, ameeleza jinsi alivyorekodi nyimbo tatu kwa usiku mmoja, akimshirikisha Nandy kwenye moja ya nyimbo hizo ambapo amesema kuwa yeye akiachwa huwa anaandika sana. "Kama mnavyojua nikiwa kwenye kipindi kama hiki peni yangu inavyokuwaga ya moto. Msichelewe kuniacha kwa maslahi mapana ya muziki wetu na taifa Kwa ujumlac Recorded 3 songs one nightpacha wangu So Chaupole na post soon unanijua nikishalewa kama hii ya @officialNandy BOMB0 CLAAAAAAA O" aliandika Harmonize. Ikumbukwe kuwa mashabiki na wadau wengi wamekuwa wakisema Harmonize hutoa muziki bora zaidi baada ya kuachwa na wapenzi wake, hali inayoonekana kumchochea zaidi katika kuandika na kuimba muziki mzuri.

Luis Miquissone arejea kwenye makali yake UD Songo

Picha
Winga wa Mpira Luis Miquissone toka ajiunge na UD Songo akitokea mitaa ya Msimbazi Kariakoo amekuwa na kiwango bora sanaa kwenye ligi kuu ya Msumbiji. Mpaka sasa Miquissone amecheza mechi 6 akiwa amefunga mabao manne, pia ameshinda tuzo 3 za mchezaji bora wa mechi Ikumbukwe Miquissone alikuwa anaichezea Simba SC kwa mafanikio makubwa kabla ya kujiunga na Al Ahly ya Misri ambayo iliachana nayo na kurejea tena Simba kisha kumuacha kabla ya kurejea kwao Msumbiji Fo

Nyota wa Simba SC ataka lawama zote Taifa Stars apewe kocha na si wachezaji

Picha
Mchezaji wa zamani wa Simba SC na kocha wa Friends Rangers Said Msasu amewataka wapenzi na mashabiki wa soka nchini kutowalaumu wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars kutokana na kipigo cha mabao 2-0 toka kwa DR Congo na isipokuwa lawama zote zipelekwe kwa benchi la ufundi la timu hiyo. "Wadau naomba nitoe maoni yangu mpira ni mchezo wa wazi makosa yake yanajirudia Tanzania tumepoteza nyumbani dhidi ya DR Congo naomba Watanzania tusilaumu wachezaji hasa kapteni Mbwana Samatta na Ally Salim". "Sio sahihi wakulaumiwa ni benchi la ufundi walitakiwa liwe na game plan kila mechi ina uchezaji wake away na home na aina ya wachezaji na line up na sub haiwezekani tunatafuta goli inafanyika sub ya kutoa", alilalamika Msasu. Said Msasu, mchezaji wa zamani wa Simba SC

Alikamwe: Simba wasibadili msemo wao ubaya ubwela Jmosi

Picha
ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapinzani wao wasibadilishe maneno waendelee na kasi yao ileile ambayo walianza nayo mwanzo wa msimu kwa kutamba na sera yao ya Ubaya sijui nini kwani Oktoba ipo karibu. "Wale ndugu zetu naona wameanza kuwa na heshima kidogo eti wanasema tunakwenda kukutana na timu kubwa, nilishangaa wao wakusema Yanga timu kubwa tangu lini? Walianza ubaya nini saizi naona wamepoa, sasa waendelee wasibadili maneno. "Mwanzo wa msimu walijua kwamba hakutakuwa na Dabi, yale majina yao wanayotuita sijui Memkwa, wakina nani waite tena halafu tukikutana uwanjani tutawaonyesha kwa vitendo,".

Abdulrazack Hamza kuikosa Yanga Jmosi

Picha
Huenda Abdulrazack Hamza (21) akaikosa dabi ya Simba na Yanga kwani leo hajaanza mazoezi na Simba Sc tangu alipopata majeraha madogo ya nyama za paja akiwa na timu ya Taifa. Hakuna matarajio ya kurejea kwake mazoezini leo Jumanne Agosti 15 wala kesho Agosti 16. Possibly, anaweza kuikosa Derby Oktoba 19. . #sokamagicupdates

Stars yafa nyumbani

Picha
Mabao mawili yaliyofungwa dakika za majeruhi na Meshack Elia dakika ya 87 na 90 yametosha kuipeleka AFCON timu ya taifa ya DR Congo baada ya kuilaza nyumbani timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa mabao 2-0 uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo DR Congo imefikisha pointi 12 ikicheza mechi nne huku Tañzania ikibaki nafasi ya pili na pointi zake nne ingawa nafasi bado inayo ya kufuzu. . MSIMAMO WA KUNDI H. . 01. 🇨🇩 DR Congo — 12 pts 02. 🇹🇿 Tanzania — 04 pts 03. 🇬🇳 Guinea — 03 pts* 04. 🇪🇹 Ethiopia — 01 pt*

Edo Kumwende aipa nafasi Yanga kwa MC Alger

Picha
Yanga dhidi ya MC Alger? Inanikumbusha mechi ya Yanga na Club Africain. Inanikumbusha pia mechi za Simba na Wydad Casablanca. Yanga ilishinda kwa Waarabu kwa bao la Aziz Ki katika mechi ambayo iliupiga mpira mwingi. Lakini tazama mechi za Simba na Wydad. Kuanzia Temeke hadi Casablanca hazikuwa ngumu. . Waarabu wana mashabiki wanaotisha lakini kwa sasa wana timu za kawaida tu. Bingwa wao aliyepita kabla ya huyu USM Alger alipata wakati mgumu kwa Yanga katika mechi zote mbili. . Fainali ya kwanza Yanga walijichanganya Dar es salaam wakachapwa 2-1. Fainali ya pili wakashinda moja bila pale Algiers. Sioni kama Yanga wanatishwa na timu za Afrika Kaskazini kwa sasa. Yanga hii ya akina Pacome ni ya moto. Ina wachezaji wengi wenye maarifa mengi.”

TP Mazembe yashitakiwa FIFA kwa kumteka mchezaji

Picha
Klabu ya TP Mazembe imeshitakiwa FIFA kwa ‘kumteka nyara’ mshambuliaji Fily Traore raia wa Mali. . Traore alishinda kesi dhidi ya TP Mazembe ambao walikuwa wanamzuia asijiunge na klabu ya Al Swehli ameishitaki tena klabu hiyo FIFA huku akidai analazimishwa kufanya mazoezi na kucheza baadhi mechi ilhali dhamira yake ni kuondoka. . Traore anadai kuwa TP Mazembe imewatuma wahuni kumpora Passport na kumlazimisha kucheza kinyume na mapenzi yake.

Timu ya taifa ya Zambia kwawaka moto

Picha
Katika hali isiyo ya kawaida mchezaji wa timu ya Taifa ya Zambia Evans Kangwa ameondoka kwenye kambi ya timu yake ya Taifa wakati wakijiandaa kusafiri kuelekea Younde Cameroon kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Chad katika kampeni ya kufuzu AFCON 2025 Mshambuliaji huyo ambaye anakipiga katika timu ya ligi kuu ya China amewaaga wachezaji wenzake na kuwaambia haoni sababu ya kuendelea kuwepo kambini ni sawa na kupotez muda ni bora akaipambanie klabu yake huko China. Kangwa amewaambia viongozi wa chama cha soka nchini humo kwamba amechagua kutoenda Cameroon kwa sababu mbali mbali ikiwemo umuhimu wake kwenye klabu yake. Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa mshambuliaji huyo ni kwamba amechukizwa na kitendo cha kocha Avram Grant kumuweka benchi katika mechi ya nyumbani dhidi ya Chad ambapo mshambuliaji Kennedy Musonda alicheza kwa dakika zote 90 Zambia itakabiliana vikali dhidi ya Chad jumanne hii ugenini huko Cameroon katika kuwania nafasi ya kufuzu AFCON nchini Morocco Ikumbukwe

Abdulrazak Hamza arejea mazoezini Simba

Picha
Beki Wa Klabu ya Simba Abdulrazack Hamza ambaye Aliondoka kwenye Kambi ya Timu ya Taifa Tanazania Kutokana na Majerhaa Ni Rasmi Amepona Majerhaa Yake na Kuanza Mazoezi na Kikosi Cha Simba Sc kinacho Jiandaa kuwakabili Yanga SC siku ya Juma Mosi October 19.

Gamondi awaandalia mvua ya magoli Simba

Picha
Kocha wa Yanga SC Miguel Gamondi raia wa Argentina amesema watacheza kwa nidhamu kubwa kuwaheshimu wapinzani wao Simba SC Jumamosi lakini anawaandaa vijana wake kushinda kwa idadi kubwa ya magoli. “Simba ni timu kubwa yenye wachezaji wenye vipaji vikubwa na historia ya mafanikio. Tunawaheshimu sana kama wapinzani, lakini tunajipanga vizuri kwa mchezo huu. . “Tunafahamu wanavyocheza na nguvu yao, lakini tutatumia maandalizi yetu kuleta ushindani na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwa kutumia nafasi kufunga mabao.”

Mohamed Salah agomea uwanja wa nyasi bandia

Picha
MSHAMBULIAJI wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah ameripotiwa kurejea England kwa kuwa hatocheza mchezo wa kesho dhidi ya Mauritania kwa sababu uwanja unaotumika umetengenezwa kwa nyasi bandia. . Taarifa ya FA ya Misri ilisema: “Benchi la ufundi likiongozwa na meneja Hossam Hassan walifanya mazungumzo na Mohamed Salah na wakaafikia kumpumzisha kwenye mechi ijayo sababu hali ya kiwanja na uchezaji wa Mauritania vinaweza kumsababishia majeraha.” . Mchezo huo wa kesho unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Cheikha Ould Boidiya wenye uwezo wa kuingiza watu 8,200 ambao unapatikana jijini Nouak-chott.

Nigeria wasusia Hiace badala ya bus

Picha
Timu ya Taifa ya Nigeria ikiwa njiani kuelekea nyumbani baada ya kuiarifu CAF kuwa wachezaji hawako tayari kucheza mechi ya Kufuzu Afcon dhidi ya Libya kufuatia mkasa uliowakuta. Wachezaji wa timu ya Taifa ya Nigeria wamefikia uamuzi baada ya kukutana na madhira nchini humo ikiwemo kupewa Hiace na wenyeji wao badala ya Bus kubwa.

Nyasa Big Bullet yapiga mtu goli 22-1 Malawi

Picha
Timu ya Nyasa Big Bullet ya Malawi imeichabanga bila huruma timu ya Kumanda AS mabao 22-1 mchezo wa kuwania Castle Challenge Cup. Katika mchezo huo mchezaji mmoja wa Nyasa Big Bullet kafunga mabao manane, na haya ni mabao yao yote. 02’—⚽️ Ronald Chitiyo 08’—⚽️Chikumbutso Salima 09’—⚽️ Chawanangwa Gumbo 14’—⚽️ Precious Phiri 41’—⚽️ Chikumbutso Salima 20’—⚽️ Chawanangwa Gumbo 31’—⚽️ Chawanangwa Gumbo 33’—⚽️ Precious Phiri 39’—⚽️ Precious Phiri 45’+1—⚽️ Chawanangwa Gumbo 45’+3—⚽️ Chawanangwa Gumbo 47’—⚽️ Precious Phiri 49’—⚽️ Stanley Billiat 50’—⚽️ Precious Phiri 58’—⚽️ Precious Phiri 59’—⚽️ Stanley Billiat 70’—⚽️ StanleyBilliat 79’—⚽️ Stanley Billiat 76’—⚽️ Efraim Kondowe 80’—⚽️ Chawanangwa Gumbo 85’—⚽️ Chawanangwa Gumbo 89’—⚽️ Chawanangwa Gumbo ✅ Mashindano ni Castle Challenge Cup. Nyasa wanatinga hatua ya 18 bora. .

#TupoNaMama: Daraja la JPM Busisi kuzinduliwa Februari 2025

Picha
Muonekano wa Daraja la JP. Magufuli linalounganisha eneo la Kigongo (Misungwi) na Busisi (Sengerema) lenye urefu wa km 3 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66. Mkoani Mwanza tarehe 13 Oktoba, 2024. Daraja hili litafunguliwa kwa matumizi February 2025.

Ngorongoro Heroes yailaza Rwanda

Picha
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imemaliza ubishi baada ya kuilaza Rwanda mabao 3-0 mchezo wa kufuzu mataifa Afrika AFCON kupitia CECAFA. Huu ni ushindi wake wa tatu mfululizo, mabao ya Ngorongoro Heroes yamefungwa na Zidane Sereli na Sabri Kondo aliyefunga mawili Ngorongoro Heroes inanolewa na mchezaji na kocha wa zamani wa Yanga, Charles Mkwasa

Taifa Stars yaendelea kujifua Kurasini

Picha
Timu ya taifa, TaifaStars ikiendelea na mazoezi kwenye uwanja wa TRA, Kurasini kujiandaa na mchezo wa marudiano kufuzu AFCON 2025 vs DR Congo. Mchezo huo utapigwa Jumanne katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Diamond Platnumz ajitabiria kifo chake

Picha
MwimbajiDiamondPlatnumz amefunguka baada ya yote ambayo yanaendelea mitandaoni. Kupitia insta story yake leo, Chibu ameweka picha iliyoambatana na wimbo wa Drake “Legend” toka kwenye Mixtape yake “If Your Reading This It’s Too Late” ya mwaka 2015. Ujumbe alioukusudia Diamond Platnumz toka kwenye mistari ya ngoma hiyo ni kwamba, hata siku akifariki na kuondoka duniani, anachokifahamu ni kwamba yeye ni Legend na ameacha alama kwa sababu ni kijana mdogo ambaye anaiwakilisha nchi.

Mume wa Zari amchakaza kwa masumbwi JK

Picha
Mume wa Zari Hassan, Shakib Chams ameshinda pambano lake la ndondi dhidi ya mwanahabari maarufu wa Uganda JK Kazoora Jumamosi usiku. Shakib hata hivyo alishinda baada ya Kazoora kujisalimisha na kumfanya mshindi wa mechi hiyo na kuzawadiwa kiasi pesa za Uganda Milion 10. Baadhi ya mashabiki wanakisia kuwa huenda matokeo ya mechi hiyo yalipangwa, Hafla hiyo ilijaa mashabiki na watu mashuhuri miongoni mwao akiwamo Zari Hassan ambaye alienda kumuunga mkono mumewe. Kumbuka kuwa miezi michache nyuma Mwimbaji @harmonize_tz alionyesha DM kutoka kwa Shakib ambaye alimtaka mwimbaji huyo kuingia naye kwenye ulingo kama njia ya kutafuta pesa. Harmonize alishiriki Meseji hizo na ujumbe kwa Zari kuwa "Zari unafahamu hili? Mtu wako anajaribu kucheza na kifo," alisema

Viwango vya wachezaji wa nje wa vilabu vya Yanga, Simba na Azam

Picha
KUANZIA tarehe 11-13 mwezi huu wachezaji wengi wa kimataifa wanaocheza Tanzania walikuwa kwenye majukumu ya kuyatumikia mataifa yao.  Nimekusogezea machache waliyoyafanya nyota hao kutokea Ligi Kuu yakiwemo mabao na Assist zao kwa Video. . WACHEZAJI WANAOCHEZA YANGA SC Uganda. Khalid Aucho (Dakika 90) vs South Sudan Kennedy Musonda (Dakika 90) Zambia vs  Chad Zambia.  Clatous Chama (Dakika 63) vs Chad Stephanie Aziz Ki (Dakika 68) Burkinafaso vs Burundi Mali. Djigui Diarra (Dakika 90 na Clean Sheet) vs Guinea Bissau  Prince Dube (Dakika 21) vs Namibia  Duke Abuya (Dakika 78) vs Cameroon . WACHEZAJI WANAOCHEZA SIMBA SC  Steven Mukwala (Hakuingia) vs South Sudan Moussa Camara (Dakika 90) vs Ethiopia . WACHEZAJI WA SINGIDA BLACK STARS . . Marouf Tchakhei (Dakika 1) Togo vs Algeria Mohamed Kamara (Dakika 90) vs  Ivory Coast . WACHEZAJI WANAOCHEZA NAMUNGO FC  Jonathan Nahimana (Dakika 45) vs  Burkina Faso

Kipa wa Simba afunika Guinea

Picha
Mlinda mlango wa Simba SC Moussa Camara jana alianza kwenye kikosi cha kwanza na timu ya taifa ya Guinea na kuisaidia kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ethiopia. Camara alicheza dakika zote 90 alifanikiwa kucheza saves 4, Camara alikuwa akisotea benchi huku timi yake ikipoteza mechi zote mbili dhidi ya DR Congo na Tanzania

Duchu alikubali benchi

Picha
Beki wa kulia wa Simba David Kameta ‘Duchu’ amesema kama mchezaji anatamani kucheza lakini mchezaji anaepata nafasi ya kucheza mara kwa mara Shomari Kapombe anatekeleza vizuri majukumu kwenye eneo lake ndio maana anaendelea kucheza mara kwa mara. Duchu ameongeza kuwa bado hajakata tamaa, anaamini ipo siku ataaminiwa na kupewa nafasi ya kucheza mara kwa mara. Eneo la ulinzi wa kulia la Simba lina wachezaji watatu, Shomari Kapombe, David Kamera ‘Duchu’ na Kelvin Kijili lakini hadi sasa bado chaguo la Kocha wa timu hiyo Fadlu Davids kimekuwa kwa mkongwe Kapombe na mara kadhaa Kijili amepata nafasi kwenye kikosi cha Simba.