Mashabiki Yanga wasiende na matokeo yao mfukoni- Masanza

“Nawakumbusha tu mashabiki wasije na matokeo yao mfukoni. Huu ni mpira wa miguu. Kama kuna mtu anaenda kuweka bondi nyumba, mke au biashara yake kwamba Singida Black Stars lazima tufungwe basi awe tayari kwa lolote.

“Tunafahamu tunaenda kucheza mechi ngumu na tutawaheshimu Yanga lakini tunao uwezo wa kupambana hadi tone la mwisho.

“Viingilio vya mechi tumeshatangaza ni shilingi 5000 (Jukwaa la Saa/Orbit) 10,000 (Jukwaa la Urusi) 15,000 (Wings) na 20,000 (VIP).

“Hii ni mechi inayokutanisha timu mbili ambazo hazijapoteza mchezo hata mmoja kwahiyo watu wasitegemee itakuwa mechi rahisi au mechi ya upande mmoja. Msimu huu tumeshasema INAWEZEKANA na tunamaanisha,”

-Massanza Jr
Afisa Habari wa Singida Black Stars.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA