Azam FC yajipigia vibonde 4-1
Azam Fc imeibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Ken Gold Fc katika dimba la Azam Complex, Chamazi kwenye mchezo wa Ligi Kuu bara na kukwea mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo.
Wanalambalamba wamefikisha pointi 18 baada ya mechi 9 huku wakifunga jumla ya magoli 13 na kuruhusu mabao matatu mpaka sasa msimu huu.
Ken Gold Fc wanaendelea kuburuza mkia, pointi 4 tu baada ya mechi 9 huku wakiruhusu jumla ya magoli 17 huku wakifunga magoli manne tu.
Mabao ya Azam FC yamewekwa wavuni na Feitoto dakika ya 20, Blanco dakika ya 38, Sillah dakika ya 50, Sidibe dakika ya 72 na Ibrahim kwa penalti dakika ya 87