Kipa Mamelodi Sundowns akosa tuzo
Golikipa wa klabu ya Mamelodi, Ronwen Williams amekosa tuzo ya kipa bora wa mwaka wa dunia na hivyo kumaliza nafasi ya 9 katika kinyang'anyiro hicho, tuzo hiyo imechukuliwa na Golikipa wa Argentina, Emiliano Martinez.
Hata hivyo Ronwen Williams ameweka rekodi ya kuwa golikipa wa kwanza Mwafrika anayechezea katika klabu ya barani Afrika kuwania tuzo hiyo.