Kigoma kuna changamoto ya viwanja- Ahmed Ally

Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema Simba SC ni timu kubwa na ina fedha hivyo ashitushwi na changamoto ya ligi kama wanavyolia wengine.

Akielezea kuelekea Kigoma siku moja kabla ya mchezo, amedai Kigoma Ina changamoto ya viwanja vya kufanyia mazoezi hivyo mazoezi yao wamefanyia Dar es Salaam.

"Kigoma huwezi kwenda mapema zaidi kwasababu kuna changamoto ya viwanja vya mazoezi, hakuna viwanja vya mazoezi kabisa kwa hiyo lazima ufanye mazoezi Dar es Salaam halafu ndio uende Kigoma siku moja kabla ya mchezo ufanye mazoezi uwanja wa mechi"

"Kama kuna mtu alipata wakati mgumu katika uwanja wa Lake Tanganyika hao ni wao kulingana na uwezo wao na ubora wao, Sisi ni Simba Sports Club na Lake Tanganyika ni ya kwetu,"

Ahmed Ally
>>Afisa habari wa Simba SC


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI