Pacome Zouzoua aimaliza Singida Black Stars
Hatimaye Yanga SC usiku huu imekamata usukani wa Ligi Kuu bara kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu baada ya kuilaza Singida Black Stars bao 1-0 uwanja wa New Amaam Zanzibar.
Shughuli haikuwa nyepesi kwani iliwachukua dakika ya 67 Pacome Zouzoua kuifungia Yanga bao pekee lililoimaliza kabisa Singida Black Stars na kuifanya ipoteze kwa mara ya kwanza.
Yanga sasa ndio timu pekee haijapoteza hata mchezo mmoja na ikiongoza kwa pointi 24 ikicheza mechi 8 ikiwa haijaruhusu goli
FT: SINGIDA BS 0-1 YANGA SC
67’—⚽️ Pacome Zouzoua