Waziri Junior mechi 6 goli moja
Mshambuliaji wa Dodoma Jiji,Waziri Junior gari bado halijawaka,Mpaka sasa amefunga bao moja tu katika michezo sita waliyocheza mpaka sasa.
Msimu uliopita akiwa viunga vya Kinondoni "KMC" Alifanikiwa kumaliza msimu akiwa na mabao 12 kibindoni na kuwa mshambuliaji namba tatu katika orodha ya wafungaji baada ya Aziz Ki na Feisal salum.
Muda bado upo wa kutosha kuonyesha uwezo wake wa kupachika mabao,Ni juhudi na kutumia nafasi zinazopatikana kwani Dodoma Jiji ina wapishi wazuri sana msimu huu eneo la kiungo.