Yanga na Azam kupigwa Chamazi
Mchezo baina ya Young Africans dhidi ya Azam utachezwa katika uwanja wa Azam complex-Chamazi badala ya Benjamini Mkapa,Sababu ya mabadiliko haya ni marekebisho makubwa yanayoendelea kufanyika katika uwanja wa Mkapa.
Mchezo huu utachezwa Novemba 2,2024,Uwanja wa Benjamini Mkapa unaendelea kuboreshwa tayari kwa ajili ya michuano ya CHAN 2025 ambayo yatafanyika kuanzia Februari 2025 katika nchi za Tanzania,Kenya na Uganda.
Aidha maboresho hayo ni sehemu ya maandalizi pia ya AFCON 2027 ambayo itachezwa katika ardhi ya Tanzania,Kenya na Uganda.