Pacome, Kibwana wahusishwa na Simba msimu ujao
Taarifa zenye uhakika ni kwsmba klabu ya Simba SC inataka kuibomoa Yanga SC kwenye dirisha kubwa la msimu ujao kwa kuwachukua nyota wake wawili kwa mkupuo.
Bilionea wa Simba, Mohamed Dewji ameweka mezani mamilioni ya shilingi akitaka kuwasajili kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua raia wa Ivory Coast na beki wa pembeni mzawa Kibwana Shomari.
Pacome kwasasa hana furaha kwenye kikosi cha Yanga na tayari ameikataa ofa ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu bara huku Kibwana anaendelea kusotea benchi.
Simba imewadhihirishia kuwasajili msimu ujao kwakua mikataba yao inaelekea kumalizika mwishoni mwa msimu