Msuva aanza kwa kishindo Irak
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ameanza msimu kwa kishindo huko Iraq baada ya kufunga bao lake la kwanza akiwa na timu ya Al-Talaba SC iliyoshinda mabao 2-0 dhidi ya Al-Karma katika mchezo wa Ligi Kuu.
.
Bao hilo la Msuva limeweka matumaini mapya kwa Al-Talaba ambao kwa sasa wapo nafasi ya sita katika msimamo wa ligi hiyo maarufu kama Stars League, wakiwa na pointi saba baada ya michezo minne, tofauti ya pointi tatu pekee na vinara, Al Shorta ambao wana pointi kumi.
.
Katika mchezo huo, Msuva alipenya ngome ya Al-Karma na kufunga kwa ustadi. Mashabiki wa Al-Talaba walimshangilia kwa nguvu, wakitambua umuhimu wa nyota huyo katika kufanikisha ushindi wa timu yao.