Kocha Azam FC wadai kuchukua ubingwa msimu huu
"Tuna furaha kwa ushindi kwa sababu tunazidi kupaa juu ya msimamo, nimekitengeneza kikosi na naona kimeanza kunipa kile ambacho nilikuwa nahitaji.
Nataka timu yangu icheze mpira wa kasi, wachezaji wangu wasikae na mpira sana, mara moja wameuachia, lakini pia wajitoe na kupambana, tukifanya hivi tunaweza kutwaa ubingwa ambao upo wazi, yoyote anaweza kuchukua, hata sisi msimu huu kwa kikosi hiki tunaweza kuupata,"
Alisema Kocha mkuu wa Klabu ya Azam Rachid Taoussi.