Yanga yaikimbiza Singida Black Stars kileleni

Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga SC imeendelea kuifukuza Singida Black Stars kileleni baada ya jioni ya leo kuilaza bao 1-0 Coastal Union mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na mshambuliaji wake Jean Baleke dakika ya 25, kwa matokeo hayo Yanga inashika nafasi ya pili nyuma ya Singida Black Stars ikiwa na pointi 21 wakati Singida ikiwa na pointi 22.

Yanga na Singida zinakutana Jumatano New Amaan Stadium, Zanzibar ambapo itajulikana nani mbabe akae kileleni, Yanga pia imeweka rekodi ya kucheza mechi 6 bila kuruhusu bao


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA