AS Maniema wagomea wachezaji wake kwenda timu ya taifa
Uongozi wa klabu ya AS Maniema Union umekitaarifu chama cha soka nchini Congo kwamba hawatawaruhusu wachezaji wao 8 walioitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Congo ambayo itaweka kambi jijini Kinshasa.
Uongozi wa klabu ya @asmaniemaunion Umesema, uamuzi huo ni kutokana na klabu hiyo kuwa na majukumu mazito ya kushiriki mchuano wa ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi ambayo itaanza kutimua vumbi mnamo Novemba 26, 2024.
As Maniema imesema itatoa ushirikiano wa kutosha kwa wachezaji wake kushiriki shughuli za timu ya Taifa kwa baadaye lakini kwa sasa ratiba hairuhusu.
Wachezaji walioitwa ni :-
Osée Ndombele
Dieu-Merci Lupini
Charve Onoya
Rachidi Musinga
Agée Basiala
Jeancy Mboma
Jephté Kitambala
Brudel Efonge