Gamondi alia na ugumu wa ratiba Yanga

Kocha wa Yanga SC Miguel Gamondi amekiri kuwa na ratiba ngumu ambayo inawapa wakati mgumu ili kuweza kutoboa lakini anafurahi sana kwa kuweza kupata angalau muda wa kupumzika-.

Yanga inakabiliwa na mechi tatu ngumu dhidi ya Coastal Union (imechezwa leo) Singida Black Stars na Azam FC, zikiwa mfululizo.

"Nimefurahi sana kuwa Arusha tena, kiukweli tuna ratiba ngumu kidogo, tumejaribu kupangilia ratiba yetu tupate angalau muda wa kupumzika.

Hatupaswi kulalamika isipokuwa kupambana na hali halisi, ingawa ukweli ni kwamba hii sio ratiba nzuri ya kujiandaa na mchezo” Miguel Gamondi


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA