Mokwena mambo magumu Wydad
Kocha mkuu wa Wydad Casablanca Rulani Mokwena baada ya kipigo cha magoli mawili juzi kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya COD Meknès kwenye Ligi kuu nchini Morocco amekiri mambo ni magumu kwake na timu yake kwa ujumla na kuomba Mashabiki wa timu hiyo wawe na subira kabla ya timu yao kuanza kufanya vizuri.
“Imekuwa ni misimu miwili migumu sana, watu wanapaswa kuelewa kwamba, wachezaji, makocha, viongozi hatuwezi kuja HAPA na kufanya uchawi, kila kitu kinahitaji muda” Alisema Rhulani.