Yanga walivyowasili Zanzibar kuwafuata Singida Black Stars leo
Kikosi cha Yanga kimefika salama visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars.
Kesho Jumatano, Oktoba 30 Yanga itashuka katika uwanja wa New Amaan Complex kumenyana na Singida BS katika mchezo wa kuamua hatma ya nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi.
Baada ya mchezo dhidi ya Singida BS, Wananchi watarejea Dar kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Azam FC utakaopigwa Jumamosi, Novemba 2