Kibwana Shomari: Sihami Yanga mniache
Mlinzi wa kulia wa klab ga Yanga , Kibwana Shomari amewaasa wadau wa mpira kunyamaza kimya na kumuacha Kocha wake Mkuu Miguel Gamondi afanye kazi, kwani anajua kile anachokifanya na ikimpendeza Kocha wake huyo Mkuu atampa nafasi ya kucheza, lakini maslahi ya timu yatangulizwe kwanza,
Akiongea Kibwana Shomari, ameeleza kuwa
" Naomba Wasinigombanishe na kocha wangu tumuache afanye kazi yake, ikimpendeza atanipa nafasi ya kucheza, kwanza timu, mengine baadaye. "
Kauli hiyo inakuja baada ya watu wengi kumlaumu Kocha Mkuu wa klab hiyo Miguel Gamondi kuwa hampi namba mchezaji huyo mwenye kipaji kikubwa.