Yanga sasa kucheza na bingwa wa Kagame, wiki ya Wananchi
Klabu ya Yanga imetangaza kwamba watacheza dhidi ya Mabingwa wa Michuano ya KAGAME Cup,Red Arrows kutoka Zambia kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi kitakachofanyika Agosti 04,2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Awali klabu ya Yanga iliwaandikia maombi Wydad Casablanca ili kusudi wakutane nao katika wiki ya Wananchi lakini imeshindikana na sasa watakutana na mabingwa wa kombe la Kagame Cup, Red Arrows ya Zambia