Ahmed Ally abeba tuzo za WAKITA
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba SC Ahmed Ally ametunukiwa tuzo ya heshima ya matumizi fasaha ya lugha ya kiswahili kutoka kwa Watetezi wa Kiswahili Tanzania (WAKITA).
Katika hafla ya utoaji tuzo kwa watetezi wengine wa lugha ya kiswahili, mgeni wa heshima alikuwa Rais mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Dkt Jakaya Kikwete ambaye pia alimkabidhi tuzo hiyo