Mangungu aongoza Ibada ya kuunusuru uongozi Simba usipinduliwe
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC Murtaza Mangungu hii leo ameongoza dua ya kuwaombea viongozi wa klabu hiyo pamoja na timu kufanya vizuri kuelekea kwenye msimu mpya wa 2024 - 25
Dua hiyo imefanyika katika uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju.
Simba imeamua kufanya dua hiyo kutokana na mwenendo wake kuwa mbaya msimu uliopita na kuambulia nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu bara huku ikitolewa Ligi ya mabingwa hatua ya robo fainali