Kocha Simba aingia shaka na kikosi chake
Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC Premier League na Kombe la Shirikisho Barani Afrika,
Davids Fadlu amesema kwa sasa anahitaji na timu iliyokamilika.
Kwasasa Fadlu anahitaji awe na timu iliyotimamu kwa ajili ya kukabiliana na michezo mbalimbali katika michuano ambayo Simba Inashiriki
"Itakapofika Siku ya Simba Day tutakuwa na wiki ya 4 na nusu ya pre season,na bado hatupo Fit kucheza dakika 90 za mchezo wa mpira wa miguu kwa sababu bado pia tunaunda Patterns mpya ndani ya timu
"Itafikia Mpaka Wiki ya 6 ambapo tutakuwa tunaanza mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu NBC.
Ni lazima tujipe muda kwa vile timu ni mpya kabisa,bado tunaunda timu kwa hivyo itatulazimu kufanya makosa kwa sababu tunatengeneza kitu kipya,tunahitaji kuwa na subira tu kwa sasa na tuende katika utaratibu mzuri alisema Fadlu