House girl wangu alinipa wazo la kujenga- Wolper
"Mimi wazo la kujenga nyumba nililipata kwa house girl wangu, nilikuwa namlipa mshahara kumbe alikuwa anatunza hadi siku aliyokuja kuniambia "Dada nashukuru kwa msaada wako mimi nimejenga nyumba kupitia mshahara wako"
Hapo ndipo akili ikanijia kuwa kumbe hata mimi naweza kujenga nyumba kwa kusevu pesa kidogo kidogo"
"Tangu hapo nilianza kusevu pesa kwa ajili ya nyumba na hatimae nikafanikiwa kujenga nyumba kubwa, nzuri ambayo thamani yake huenda ni zaidi ya shilingi milioni 500 za Tanzania ingawa bado haijaisha vizuri.
Namshukuru house girl wangu kwa kunipa wazo" - Jacqueline Wolper, mwigizaji maarufu Tanzania pia mfanyabiashara