Msimu ujao Yanga itaalikwa Ulaya- Dauda
Mchambuzi wa michezo Shafih Dauda amesema hatoshangaa msimu ujao klabu ya Yanga ikialikwa barani Ulaya kwenye mechi za pre season na hasa kutokana na kwenda nchini Afrika Kusini.
"Nimefuatilia Pre Season ya Yanga kwa maana maandalizi yao ya msimu mpya wakiwa hapa nyumbani na baadae kwenda Afrika Kusini kwa mualiko maalumu na hivi vitu haviji tu ni lazima kuna mbegu unakuwa umeipanda baada ya muda ndio unaona shina na matunda yake , Yanga wamefanikiwa kwenye hilo hasa matokeo ya jumla ya mechi zao"
"Hii imefanya wauze sana na sitoshangaa kama msimu ujao watapata mialiko mingi zaidi" amesema Shafih Dauda