Ayoub Lakred nje miezi 6
Golikipa, Ayoub Lakred atakaa nje ya uwanja kwa miezi sita. Simba SC imeshakamilisha usajili wa golikipa mwingine, Moussa Camara kutoka Horoya AC.
Ayoub ataondolewa kwenye mfumo wa (CAF) ili kumpisha kipa mpya kwa sababu idadi ya wachezaji wa kigeni itazidi.
Aishi Manula hana maelewano mazuri na uongozi wa Simba SC hivyo ni ngumu kurejea kikosini. Anashutumiwa kwa kufungwa bao 5-1 na Young Africans Sports Club.