Simba wasimng' ang' anie Kibu- Rage
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amewaomba viongozi wa Simba SC kutomng'ang'ania winga, Kibu Denis.
"Kibu Denis ameonyesha kutokuwa mwaminifu na huenda akawa sehemu ya wahujumu Simba SC msimu unaofuata.
Viongozi wa Simba hawapaswi kumng'ang'ania na nawasihi viongozi wa Simba wasimkomoe mchezaji bali atakaporejea wazungumze naye ili kila upande unufaike kulingana na makubaliano lakini wamruhusu aende zake."
"Mimi niliwahi kukutana na kesi kama hiyo nilipokua katika harakati za kumsajili Mbuyu Twite ambaye licha ya kumpatia dola elfu (40) lakini akasaini pia na Yanga SC ambapo ili kuepusha mgogoro tulimueleza arudishe pesa tulizompa na kuongezea dola elfu tano" alisema Rage