Gamondi amduwaza Nabi, Yanga ikiichapa Kaizer 4-0
Yanga SC chini Miguel Gamondi jioni ya leo imeichapa Kaizer Chief inayonolewa na Kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi mabao 4-0 kwenye uwanja wa Toyota mchezo wa kuwania kombe la Toyota.
Prince Dube dakika ya 25 amefungua ameendelea kufunga baada ya kuiandikia bao la Kwanza kabla ya Stephanie Aziz Ki dakika ya 45 kufunga bao la pili.
Clement Mzize dakika ya 57 alifunga bao la tatu kabla ya Aziz Ki ambaye leo ameshinda tuzo ya mchezaji bora, Aziz Ki alifunga bao hilo dakika ya 62.
Baada ya ushindi huo Yanga imetawazwa kuwa mabingwa wa Toyota Cup