Mzee Magoma azidi kumkalia kooni Injinia Hersi
Pale Yanga SC kuna makundi ukionekana wewe siasa zako zinaenda kinyume na wao wanakuweka pembeni. Mimi siwezi kuwa mtumwa wao hata siku moja nitaendelea kusimamia kwenye katiba.
Kwa sasa siwezi kwenda pale klabuni kwasababu nimeomba serikali inirinde sasa nikienda pale wakati nimeshawasha moto si itaonekana nimejitakia.
Mimi nimekataa kutumika kama wengine,hauwezi kuona nimekaa pale nasuburi viongozi wanipe mia mbili, amesema mzee Magoma