Kocha Simba amtupia virago Onana
Wakati jana Mambo Uwanjani Blog ikimnukuu kocha wa Simba Fadlu Davids kwamba hana imani na kikosi chake kilichopo Ismailia, Misri.
Leo kocha wa klabu hiyo Fadlu Davids ameuomba uongozi wa Klabu kumtafutia mbadala wa Mchezaji Willy Essomba Onana kwani ameonekana kutokufurahishwa na namna Mchezaji huyo anavyosakata Kabumbu.
Na hii inafanya kutimia idadi ya wachezaji watatu waliokataliwa na Kocha Fadlu akiwemo Freddy Michael na Ayoub Lakred kutokana na uzito mkubwa hadi kulazimika kumuanzishia Programu ya pekee yake ili kurudisha utimamu wa mwili iliyomfanya kupata majeraha Kipa huyo.