Paul Godfrey Boxer atua Songea United
Beki wa zamani wa Yanga, Paul Godfrey ‘Boxer’ amejiunga na Songea United (zamani FGA Talents) iliyopo Ligi ya Championship, ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.
Uongozi wa timu hiyo umeona kiwango cha Boxer, kitawasaidia kutokana na uzoefu wake alionao baada ya kucheza timu tofauti za Ligi Kuu ambapo msimu ulioisha alikuwa Ihefu (sasa Singida Black Stars).