Debora amfunika mbaya Ngoma na kutakiwa aondoke kikosini
Siku za mchezaji wa Simba SC Fabrice Luamba Ngoma raia wa DR Congo zinahesabika kwani tayari kocha wa klabu hiyo Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini ameshamkataa na anataka atupiwe virago.
Lakini adui wa maisha ya Ngoma aliyesajiliwa kwa madaha msimu uliopita ni kiungo mpya kutoka Angola mwenye uraia wa Congo Brazaville Debora Fernandez Mavambo ambaye amekuwa akikichafua vibaya mno kiasi kwamba kocha anamuona Ngoma kama mzululaji uwanjani