Dube afungua akaunti ya mabao Yanga ikiichapa TS Galaxy
Timu ya Yanga SC ya Tanzania jioni ya leo imeifunga timu ya TS Galaxy ya Afrika Kusini bao 1-0 katika uwanja wa Kalamazane katika mchezo wa michuano ya Mpumalanga Primier.
Bao pekee la Yanga limefungwa na mshambuliaji wake mpya Prince Dube dakika ya 55, huo ni mchezo wake wa pili baada ya mechi ya kwanza kufungwa mabao 2-1 na Ausburg ya Ujerumani.
Yanga itashuka tena uwanjani siku ya Jumapili ikichuana na Kaizer Chief pia ya Afrika Kusini kuwania kombe la Toyota